Moyo Wangu

Wanasema ukikalia kuti kavu kuanguka sio ajabu
Na ukikaa na mpumbavu hupati kitu ila aibu
Unajifanya mjanja kwa marafiki zako
Ukisema nalilia kwako umenifunika
Tena unajipendekeza zako misifa
Majivuno ukipita habari magazeti
Kumbe mkongwe mkoma asiyejiweza
Mkongojo nakupa sayari kwangu hupati

Mara kunipa majina kwa marafiki kunishombokea
Aty sina lolote mtoto bado mchanga
Jaribu jikaze nitakukera kwa sana
Nyota inazidi kung'aa mtoto amekua

Moyo wangu husiwaze kiduchu
Moyo wangu kidoto wangu haukamatiki
Moyo wangu ubati bure utajiumiza
Moyo wangu bayana mlango nimeweka bawabu

Tena kiburi kifua kujifurisha
Mara vyumba vya kifahari magari unamiliki
Manneno kasuku unaropokwa
Mwingereza utengeneza akakereza
Penzi lenye uhondo mwisho wake uvundo
Unajiona mrembo ulimbo ungali njiani
Unapendeza shwari umekamilika mazima
Ila tatizo kidoa unaharibu za wenzako

Mara kunipa majina kwa marafiki kunishombokea
Aty sina lolote mtoto bado mchanga
Jaribu jikaze nitakukera kwa sana
Nyota inazidi kung'aa mtoto amekua

Moyo wangu husiwaze kiduchu
Moyo wangu kidoto wangu haukamatiki
Moyo wangu ubati bure utajiumiza
Moyo wangu bayana mlango nimeweka bawabu



Credits
Writer(s): Danson Musyoki
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link