Miaka Ya Mbwa (feat. Liboi, Murathe Ngigi, Lexas Mshairi & Kikete FM)

Ni kama wengine wetu hatukuumbwa
Vichochoroni tunapewa vichapo vya mbwa
Barabarani tunauliwa kama mbwa
Na siku zetu maishani miaka ya mbwa
Miaka ya mbwa
Miaka ya mbwa
Miaka ya mbwa
Miaka ya mbwa

Ni sixteen miaka
Ni sixteen risasi
City ama chiromo?
Utadhani zinamiminiwa momo
Kumbe ni kijana m-slim mono
Wanasema anasumbua mtaa
Sa ameuliwa akitafutia mtu wake kimono
Ako kwa miaka yenye hajui kutofautisha hype na hustle ripe
Ako na joto ya ngono shinda venye ana joto ya masomo
Anajua kuiba sana hadi ana-feel at home akiwa ndani ya kibeti
Anashinda na kiberiti ndo anytime anaeza kiseti
Ana abuse substance kuwa zone
Ju hizi ni substance ever since akuwe born
Idea yake ya success ni kuvaa, madem na magari
Grave inakaa far-fetched
Ju wizi anaichukulia kama activity brave
Niko kwa matanga yake nikiskiza reggae
Ngoma ya Demarco "fallen soldiers" venye D hayuko
Na A for Amen yakufunga maombi kama coffin
Ni enzi ya Covid
Lakini kijana hajakufa ju ya coughing

Legacy ni
Kupanda mbegu kwa shamba hutawai see
Kama vile Dady alienda ka hajainiona
Sijui ka mama ashaipona
Juu magizani ye uniacha nyumbani anaenda mwenyewe dukani
Hataki nijitolee
Juu huenda pia mimi msiba unitokee nisirejee
Kufika nilipo nimeona mengi gathee
Ka kushukiwa na kuangushwa kwa mabrathee
Kutengwa
Juu ya place natokea
Cake ni kubwa tuliochagua hawadai ku-share
So to secure my future lazima ni-strive
Nipande mbegu for a new life
Teenage husband to my teenage wife
Majaliwa, nitakuwa around long enough
Kushuhudia my young one akizaliwa
Ama labda hii script ata ilishamaliziwa?
Thy will be done
Mkono kwa gun na bonoko kwa plan
Tumia risasi mingi
Mama lazima akujie mwili
Hizo zote zitalipiwa
Bang! Bang! Bang! BANG!

Ni kama wengine wetu hatukuumbwa
Vichochoroni tunapewa vichapo vya mbwa
Barabarani tunauliwa kama mbwa
Na siku zetu maishani miaka ya mbwa
Miaka ya mbwa
Miaka ya mbwa
Miaka ya mbwa
Miaka ya mbwa

Cheki,
Mi sikuzaliwa tao kwa esto
Sikuchomewa hao kwa ghetto
Ngware na majamaa
Tuliwinda ma-sungura
Daily ndani ya fore
Tulinyorea ma-tree
Kuchora territory
Miaka, mikaka
Tukikata tu mamiti kukuza miji
Kumbe mimi kijijini nikicheza
Jijini walisaka chuma kwa mapipa kuuza
Haba haba ijaze kibaba ya mama fua
Baba alikataa kutoka teke, akashikwa
Ju trolley yake ya mayai haikua na leseni
Watoi wanakua bila grao za kucheza ma-game
Waepuke cycles za crime kwa ma-baze
Cheki miche ya future ya nchi
Ikiachwa ikauke bila maji
Na bado cracks za ghetto
Zinaota maua kujitegemea
Kwani sisi sio mandhari fiti ya city
Kwa walami wamekuja matembezi
Tukule gas na ma-risasi
Kesi izunguke mibuyu kotini
Wanahabari waripoti
Ni kama tu ni filamu ya wiki
Kumbukumbu ya ndoto changa
Ikigeuka misalaba ya mchanga
Mwana kama tu baba
Ju eti mbwa koko
Haina haki za Chihuahua

Inaonekana
Toka genesis life yangu ilikuwa set
Kuwa more lamentations than psalms
If by any chance earth ni Garden ya Eden
Kuna wenye wanaimiliki
The likes of me scum
Our song of songs ni dirge tukiwa farewell Langata
Another of my peers amekuwa gone to never return
Another casualty of this perennial calamity
Another sacrificial lamb kwa alter ya impunity
Only thing ni Isaac akishachukuliwa
Hakuna magical appearances za miraculous rams
Hakuna fresh water fountains ama parting highways kwa dams
Ama baby Moses alizama ndani ya river labda?
Juu hakuna sign ya exodus toka hii misri ya slums
Huku Pharaoh ni karao psycho aki-finger trigger
Kuongeza numbers kwa deathlist ya sons
Ni kama tunazaliwa ndio tufe kabla boy a-turn man
Hii si parable nime-memorize kwa biblia
Rather ni everyday life ya me and my peers
Condemned to live
In dog years



Credits
Writer(s): Dennis Mutua
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link