Nasafiri

Nimekuja kuageni
Mi nimepata safari
Na sijui siku gani
Ndo najiweka tayari

Sitorudi asilani
Niombeeni ya kheri
Hilo haliwezekani
Ameshapanga Jalali

Ni nzito kwa yakini
Jamani hii safari
Sjaona abadani
Katika wangu umri

Na itapofika hii safari
Hazitonifaa zangu mali

Na watoto wangu wapeni malezi mazuri
Ndio faraja yangu dua zenu zikikithiri

Niombeeni ya kheri
Ni ngumu hii safari
Wala haina mithili
Katika zote dahari

Nasafiri kwenda mbali
Na wala sina khiari
Nimeshapewa amri
Sina budi kukubali
Nimeshapewa amri
Sina budi kukubali
Na siku haipo mbali
Nimeshaona dalili
Na siku haipo mbali
Nimeshaona dalili

Mola anifanyie Sahali
Maana naogopa kweli kweli

Hivi nitapata kheri au nitalipwa nari
Na zawadi zangu je Mola atazikubali

Mizigo ipo tayari
Ili nianze safari
Niombeeni yakheri
Nipokelewe vizuri

Nimekuja kuageni
Mi nimepata safari
Na sijui siku gani
Ndo najiweka tayari

Sitorudi asilani
Niombeeni ya kheri
Hilo haliwezekani
Ameshapanga Jalali

Ni nzito kwa yakini
Jamani hii safari
Sjaona abadani
Katika wangu umri



Credits
Writer(s): Salim Ally
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link