Subira

Subira, ah, tuwe na subira
Tujifunje kusubiri, tuwe na imani
Subira, ah, tuwe na subira
Tujifunje kusubiri, tuwe na imani, mm

Anayetoa ndo' anayetoa kwa wote
Hatuko wengi nasihi, ridhiki zetu sote
Mm-hmm, usinung'unike nafsini
Utakufuru, yamkini

(Kesho-kesho, kesho) uwenda ndio siku yako
(Kesho-kesho, kesho) usifadhaike na hali
(Kesho-kesho, kesho) omba dua fanya sala
(Kesho-kesho, kesho) iye-iye

Kila mwenye kuomba hufunguliwa
Hamtupagi mja wake
Sio mwenye kugomba, kusujudiwa
Wajibu wake Yeye

Lakini pia Ye' habagui
Mweupe au mweusi, hachagui
Kipofu au kiziwi hujitambui
Fungu lako lipo

Mm-hmm, usinung'unike nafsini
Utakufuru, yamkini

(Kesho-kesho, kesho) uwenda ndio siku yako
(Kesho-kesho, kesho) usifadhaike na hali
(Kesho-kesho, kesho) omba dua fanya sala
(Kesho-kesho, kesho) iye-iye

(Kesho-kesho, kesho) uwenda ndio siku yako
(Kesho-kesho, kesho) usifadhaike na hali
(Kesho-kesho, kesho) omba dua fanya sala
(Kesho-kesho, kesho) iye-iye

(Kimmaba on the beat)

Credits
Writer(s): Marioo Mwanga
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link