Mama Yangu Ndio Baba

Ameamka asubuhi nguo kanivalisha
Vijisenti vya jana alivyochanga vya vikoba
Nauli ndo kanipa
"Baba ameenda kazini leo tena haumuoni"

Heri abebe nawe mpende
Mjaze na faraja uso
Mimi mwanae anipa funzo
Ili niwe mpenzi wako
Nampenda mfano hana mungu baba mbariki
Mama yangu ndiye nguzo aliye na thamani
Baba kaingia mitini mimi nimekosa nafasi
Mama yangu ndio baba kwangu mimi
Nakuomba

Mama anasema
"Ameondoka nyumbani mapema"
Unawaza baba harudi kazini nawe umuone
Ila mama anasema
"Baba yako hutamuona
Siku saba hapa nyumbani hayupo"
Ila ndani analalama mtoto, matunzo
Vyake vilio usikie

Heri abebe nawe mpende
Mjaze na faraja uso
Mimi mwanae anipa funzo
Ili niwe mpenzi wako
Nampenda mfano hana mungu baba mbariki
Mama yangu ndiye nguzo aliye na thamani
Baba kaingia mitini mimi nimekosa nafasi
Mama yangu ndio baba kwangu mimi
Nakuomba Mungu

Heri abebe nawe mpende
Mjaze na faraja uso
Mimi mwanae anipa funzo
Ili niwe mpenzi wako
Nampenda mfano hana mungu baba mbariki
Mama yangu ndiye nguzo aliye na thamani
Baba kaingia mitini mimi nimekosa nafasi
Mama yangu ndio baba kwangu mimi
Nakuomba



Credits
Writer(s): Taariq Madoweka
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link