Nyakati Za Mwisho

Ni nyakati za mwisho wee
Jamani njooni tumuombe Mungu
Yeye atusaidie maana ni siku za mwisho
Ni nyakati za mwisho
Tanzania tumuombe Mungu
Maana gonjwa la ukimwi linaitikisa dunia
Taifa tumuombe Mungu eeh
Yeye atusadie maana vitendo vya ugaidi vinaitikisa dunia

Hebu fikiria ajali ya Dodoma ilivyomaliza watu, hilo naomba ujue
Hebu fikiria gonjwa la ukimwi linavyomaliza watu, hilo naomba uzuru
Hebu fikiria tena naomba kumbuka vitendo vya ugaidi vilivyomaliza

Hivi wewe na mimi
Tunapoyaona hayo tunajifunza nini kutoka kwa hao wenzetu
Au tunasubiri sala za marehemu wawaite wachungaji waje kutuombea
Je maisha yako wewe, nani atayadhamini usipomruhusu huyu Yesu
Yeye kufanyta marekebisho
Elimu yako kaka, nani ataidhamini usipomruhusu huyu Yesu
Yeye kufanya marekebisho
Ujana wako wewe, nani ataudhamini usipomruhusu huyu Yesu
Yeye kufanya marekebisho

Kinachonitia uchungu ninapowaona wapendwa wanangangania dini
Wanamkataa huyu Yesu
Kinachonitia uchungu ninapowaona wapendwa wanangangania vyeo
Wanamkataa huyu Yesu
Ukifa leo wewe nani atakudhamini usipomruhusu huyu Yesu
Yeye kufanya marekebisho
Vyeo vyako baba nani atavidhamini usipomruhusu huyu Yesu
Yeye kufanya marekebisho
Uongozi wako Baba nani ataudhamini usipomruhusu huyu Yesu
Yeye kufanya marekebisho
Maisha yako wewe nani atakayedhamini usipomruhuus huyu Yesu
Yeye kufanya marekebisho

Au unafurahishwa na yale majina ya wafu wakuite maiti wakuite marehemu
Wakuite hayati wakuite msiba au inapendeza yeye aje akusaidie
Lakini maisha yako leo nani atakudhamini usipomruhusu huyu Yesu
Yeye kufanya marekebisho
Ukifa wewe leo nani atakudhamini usipomruhusu huyu Yesu
Yeye kufanya marekebisho

Maisha yangu mimi, nani angenidhamini asingekua ni huyu Yesu
Yeye kufanya marekebisho
Maisha yangu yote, nani angenidhamini asingekua ni huyu Yesu
Yeye kufanya marekebisho
Minakushukuru Mungu, kwa upendo wako huo
Kuniokoa maisha yangu, ningekua wapi mimi?
Minakushukuru Mungu, kwa upendo wako huo
Kugharamia maisha yangu, ningekua wapi mimi?
Maisha yangu mimi nani angenidhamini, asingekua ni huyu Yesu
Yeye kufanya marekebisho
Usomi wako wewe, nani ataudhamini, usipomruhusu huyu Yesu
Yeye kufanya marekebisho
Usomi wako kaka, nani ataudhamini, usipomruhusu huyu Yesu
Yeye kufanya marekebisho
Mpokee Yesu leo, yeye katika maisha yako
Awe bwana na Mokonzi ili afanye marekebisho
Mpokee Yesu leo katika maisha yako
Awe bwana na mokonzi yeye afanye marekebisho
Mpokee Yesu leo



Credits
Writer(s): Bahati Bukuku
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link