Mapito

Mapito, ooh
Mapito, eh
Mapito, eh
Mapito
Kweli mapito, eh

Mapito kwa mjane anaponyang'anywa mali, eh
Mapito kwa wanandoa wanapofarakana
Mapito kwa wasomi wanapofukuzwa kazi, eh
Mapito kwa wachumba wanapodanganyana

Duniani kuna mapito, oh
Ambayo kweli mwanadamu anapitia
Kweli mapito, oh, yanakatisha tamaa
Kweli mapito yanavunja moyo

Duniani, eh, kuna mapito, oh
Ambayo ni kweli mwanadamu anapitia
Kweli mapito, oh, yanakatisha tamaa
Kweli mapito, mama, yanavunja moyo

Haijalishi wewe mapito yako, oh
Wewe ni mjane mama, wamekunyang'anya mali
Jibu sio kulaumu, mwamini Yesu, oh
Yeye aliyekupa mali airekebishe

Haijalishi mama mapito yako, oh
Wewe ni mjane eh, wanakunyang'anya mali
Jibu sio kulaumu, mwamini Yesu, oh
Yeye ndiye jibu lako, akusaidie, ha

Vumilia, vumilia mama
Vumilia, tena muombe Mungu
Vumilia, vumilia mama
Vumilia, huku ukimwomba Mungu
Inakupasa uvumilie mama
Inakupasa uvumilie mjane, yeh

Yawezekana baba mapito yako, oh
Iyo ndoa yako inakusumbua
Yawezekana mama mapito yako, oh
Iyo ndoa yako inakusumbua

Jibu sio talaka mama mwamini Yesu, oh
Yeye aliekupa ndoa airekebishe, eh

Yawezekana baba mapito yako, oh
Iyo ndoa yako inakusumbua
Yawezekana mama mapito yako, oh
Iyo ndoa yako inakusumbua

Jibu sio haki sawa mwamini Yesu, oh
Yeye aliekupa ndoa airekebishe, eh

Vumilia, vumilia baba
Vumilia, vumilia mama
Vumilia, vumilia baba
Vumilia, vumilia mama
Inakupasa uvumilie mama
Inakupasa uvumilie, eh-eh
Inakupasa uvumilie, eh-eh, aah

Yawezekana baba mapito yako, oh
Ni maisha magumu, eh, yanakusumbua
Jibu sio kujiua, mwamini Yesu, oh
Yeye mtuliza bahari, ayarekebishe, eh

Yawezekana mama mapito yako, oh
Ni maisha magumu, eh, yanakusumbua
Usikate tamaa, mwamini Yesu, eh
Yeye ndie jibu lako, atarekebisha

Mwamini Yesu, mwamini Yesu baba
Jibu lipo, jibu lipo mama
Mwamini Yesu, mwamini Yesu baba
Jibu lipo, jibu lipo baba

Inakupasa umwombe Mungu, eh-eh
Inakupasa umwombe Mungu, eh-eh
Mwombe Mungu, mwombe Mungu

Haijalishi kaka, mapito yako, oh
Ni huyo mchumba, ah, amekudanganya
Yawezekana dada, mapito yako
Ni huyo mchumba, ah, amekurubuni

Usikate tamaa, mwamini Yesu, eh
Kumbuka mme mwema hutoka kwa Mungu
Usikate tamaa, mwamini Yesu, oh
Kumbuka mke mwema hutoka kwa Mungu

Acha tamaa, wewe muombe Mungu
Acha tamaa, wewe muombe Mungu
Vumilia huku ukimwomba Mungu, eh
Vumilia huku ukimwomba Mungu

Inakupasa uvumile kaka
Inakupasa uvumile dada

Vumilia, tena umwombe Mungu
Vumilia, tena umwombe Mungu
Inakupasa uvumile kaka
Inakupasa uvumile dada, ah

Vumilia, vumilia baba
Vumilia, vumilia mama
Inakupasa uvumilie, eh-eh
Inakupasa uvumilie, eh-eh

Vumilia, vumilia kaka
Vumilia, vumilia dada
Inakupasa uvumilie, eh-eh
Inakupasa uvumilie, eh-eh, aah



Credits
Writer(s): Bahati Bukuku
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link