Pesa

Hadithi hadithi
Hadithi njoo, uwongo no
Sitaupokea
Zamani za kale palikuwa na jamaa pale
Alijawa tamaa
Yeye hakujali
Alipenda mali, mponda raha

Alikuwa msaka fedha
Wasichana walimpenda sana
Aling'aa

Vitu vya dhamana, havitopatikana
Kwa pesa, kwa pesa
Upendo wa maana
Hautopatikana kwa pesa
Kwa pesa

Heiye yeiye yeiye
Heiye yeiye yeiye
Heeya
Hadithi, hadithi
Endelea, ukweli pepea
Tutaupokea
Alioa mke, mrembo kati ya wake
Alibahatika
Cha kuhuzunisha
Penzi halikumtuliza
Aliranda randa
Alijulikana mjini
Ungejua h'ungeamini
Maajabu ya musa

Vitu vya dhamana, havitopatikana
Kwa pesa, kwa pesa
Upendo wa maana
Hautopatikana kwa pesa
Kwa pesa

Alikuwa msaka fedha
Wasichana walimpenda sana
Aling'aa
Alijulikana mjini
Ungejua h'ungeamini
Maajabu ya musa hee

Havitopatikana
Kwa pesa, kwa pesa
Upendo wa maana
Hautopatikana kwa pesa
Kwa pesa
Vitu vya dhamana, havitopatikana
Kwa pesa, kwa pesa
Upendo wa maana
Hautopatikana kwa pesa
Kwa pesa

Hadithi, hadithi
Hadithi njoo



Credits
Writer(s): Benjamin Webi
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link