Huniachi

Umeahidi wewe Bwana huniachi
Hadi mwisho wa dahari ulisema huniachi
Wewe ni Mungu uliye mwaminifu siku zote(hubadiliki)
Mimi naiweka Imani kwako baba

Nipitiapo maji mengi au moto huniachi
Unalijua jina langu ewe bwana huniachi
Unatengeneza njia hata mito kule jangwani
Wewe ndiwe alpha na omega huniachi

Umeahidi wewe Bwana huniachi
Hadi mwisho wa dahari ulisema huniachi
Wewe ni Mungu uliye mwaminifu siku zote
Mimi naiweka imani kwako baba

Uliwalinda wana Israeli kule Jangwani
Ukamtoa danieli kutoka tundu la simba
Wewe huwainua na wanyonge siku zote
Watuepusha na hatari kila siku usifiwe

Umeahidi wewe Bwana huniachi
Hadi mwisho wa dahari ulisema huniachi
Wewe ni Mungu uliye mwaminifu siku zote
Mimi naiweka imani yangu kwako baba

Baba hata mama wanaweza kunikana
Marafiki nao wanaweza nigeuka
Mara kwa mara maadui wanizunguka
Nitaishi kwa ahadi yako bwana, huniachi huniachi

Umeahidi wewe Bwana huniachi
Hadi mwisho wa dahari ulisema huniachi
Wewe ni Mungu uliye mwaminifu siku zote
Mimi naiweka Imani kwako baba

Umeahidi wewe Bwana huniachi
Hadi mwisho wa dahari ulisema huniachi
Wewe ni Mungu uliye mwaminifu siku zote(hubadiliki)
Mimi naiweka Imani kwako baba



Credits
Writer(s): Reuben Kigame
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link