Mbagala

Mm-mm, mm

Busara na upole, na hekima nilorithi kutoka kwa mama yangu, mama
Vyote haukuvijali, ukaona silingani kabisa kuwa na wewe
Akuti na Mkole, ukakata kabisa na shina la penzi langu, nana
Eti kisa mali, ukaona bora uniache mimi na uolewe

Ile siku shekhe namuona anachoma ubani
Unavishwa pete unakuwa mke wa fulani
N'liumia sana, sana, ah
Ile siku shekhe namuona anachoma ubani (ah-ha)
Unavishwa pete unakua mke wa fulani (ah-ha)
Niliumia sana, mi niliumia sana, sana

Tatizo kwetu Mbagala, hapa nyumba mbele jalala
Tatizo kwetu Mbagala, ukaona mapenzi siwezi
Tatizo kwetu Mbagala, hapa nyumba mbele jalala
Tatizo kwetu Mbagala, ukaona mapenzi siwezi

Ah-ah, ungejua jinsi gani
Machozi n'lolia kwa uchungu wa penzi langu, na
Mwenzio jinsi gani, vile nimeumia moyoni
Hata kupendwa sitamani
Utamu wa mapenzi mwenzako umekula kwangu, ma'
Mwenzio sitamaani, hata raha tena mi sioni

Ah, naskia hivi sasa una mtoto anaitwa Mamu
Vile akinuna mpaka atabasamu
Mmefanana sana, sana
Mi' mwenzako tena mapenzi mi' sina hamu (ah)
Tena na mpango wa kuhama Dar Es Salaam (ah)
Nataka niende mbali, niepuke visa na walimwengu
Mi' mwenzenu siwezi

Tatizo kwetu Mbagala, hapa nyumba mbele jalala
Tatizo kwetu Mbagala, ukaona mapenzi siwezi
Tatizo kwetu Mbagala, hapa nyumba mbele jalala
Tatizo kwetu Mbagala, ukaona mapenzi siwezi

Nasema Mbagala, Mbagala, Mbagala, a-ah
Mbagala, ukaona mapenzi siwezi
Nasema Mbagala (Mbagala), Mbagala (Mbagala), Mbagala (Mbagala), eeh
Mbagala, ukaona mapenzi siwezi

Tatizo kwetu Mbagala (mm, Mbagala), hapa nyumba mbele jalala (mm, mbele jalala)
Tatizo kwetu Mbagala, ukaona mapenzi siwezi
Tatizo kwetu Mbagala, hapa nyumba mbele jalala
Tatizo kwetu Mbagala, ukaona mapenzi siwezi (mama, ma', ah)

Mbele jalala (jalala), kwetu Mbagala (Mbagala)
Mm, mape-
Eh-eh, hi-hi, na, na, na, na, na, na, eh
Ayo (ayo), yo I'm Platnumz ladies, I'm back (I'm back)
The Sharobaro President, Bob Junior
Mr. Chocolate Flava
Yo, I'm back, Diamond I'm back ha-ha
Nimemaliza

Credits
Writer(s): Diamond Platnumz
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link