Kimbia

Kila mmoja wetu amepewa neema kutoka kwa Mola
Vipaji mbalimbali, katupea Muumba na pia baraka halafu pia kibali
Kila kukikucha sote tunasema asante Mungu, asante Baba
Kukipambazuka, sote twaamka, shughuli mbalimbali, huku na kule hapa na pale
Majukumu yetu na shughuli zetu na juhudi zetu kwa mkate wa kila siku
Kijana, maisha ni safari inabidi kuongeza kasi kwa mbio zako
Mwenzangu, maisha mapambano, ukiwa na kipaji wacha kuzembea
Mwisho wa siku weka chakula mezani
Kimbia, kimbilia jaami yako
Kimbia, Kimbilia taifa lako
Kimbia, Kamilisha ndoto zako
Kimbia... ooh, Kimbia
Hebu cheki, foleni za magari asubuhi mjini
Dereva wa matatu anavunja sheria kwa kuoverlap
Wanariadha kuruka viuzi na maji kupata medali
Wanasiasa wako mbioni mashinani kuuza sera zao; kupata kura
Na sisi wasanii, tunatunga mistari kupata riziki
Kijana, maisha ni safari inabidi kuongeza kasi kwa mbio zako
Mwenzangu, maisha mapambano, ukiwa na kipaji wacha kuzembea
Mwisho wa siku kijana weka chakula kwa table yako
Kimbia, kimbilia jaami yako
Kimbia, tetea ubingwa, tetea ubingwa
Kimbia, Kamilisha ndoto zako
Kimbia... ooh, Kimbia
Nikiwa mdogo baba yangu kanieleza
Enda shule mtoto upate elimu
Ukiwa na elimu utapata kazi nzuri
Akasahau kunieleza, ukuze kipaji
(.Sax playing.)
Kimbia, kimbilia jaami yako
Kimbia, kimbilia nchi yako
Kimbia, Kamilisha ndoto zako
Kimbia, kimbilia jaami yako
Kimbia, Kamilisha ndoto zako



Credits
Writer(s): Jean-pierre Nimbona
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link