Utatulia

Aye
It's Bonga
Kiangazi masika ukiichanganya
Vyote vikashuka kwangu vitanielemea
Ntakosa pa kushika ntavavanya
Wewe ndo mwandani wangu nliokuzoea
Ntunza vyangu visiri mwenye kunisitiri
Fundi mitambo
Kinga yangu ya mwili usiyelipa bili
Kuchoma changu
Simtaki kafiri jangiri mwingi wa mambo
Moyo akaukatilli
Nikondeshe mwili
Ajifanye Rambo

Si unajua
Dalili ya mvua mawingu
Ikitaka kunyesha
Huwa yanatanda
Nami si unajua aah
Nimeumbwa na wivu
Kidogo tu pressure
Yanshuka yapanda
Niahidi kama

Utatulia ah
Baby
Niahidi kama (utatulia ah)
Hmm
Nisibaki nkashika tama
Utatulia ah
Baby
Niahidi kama (utatulia aah)
Hmm
Wasiniibie cha ngama

Maneno yangu si Biblia wala Masaafu
Useme usibadili (hmm)
Jichunge kipenzi changu
Unanisikia usicheze rafu
Yatimie waliotabiri
Usijifanye Ronaldinho
Penzi utie mbwembwe
Utahaaribu
Visokolokwinyo
Wakupitie denge kukujaribu
Kina Capuchino wakakutia wenge kwa vizabibu
Wakugongeshe mvinyo
Ukaota mapembe iwe aibu

Si unajua
Dalili ya mvua mawingu
Ikitaka kunyesha
Huwa yanatanda
Nami si unanjua aah
Nimeumbwa na wivu
Kidogo tu pressure
Yanishuka yapanda
Niahidi kama

Utatulia ah
Baby
Niahidi kama (utatulia ah)
Hmm
Nisibaki nkashika tama
Utatulia ah
Baby
Niahidi kama (utatulia ah)
Hmm
Wasiniibie cha ngama

Eeeh eh
Yani kama ukitulia tulia
SItathubutu macho kupepesa
Ukitulia tulia
Ukinipa kiduchu nitatosheka
Kama ukitulia tulia
Sitofwata nguruchu niende teseka
Ukitulia tulia
Eh eh
Nami ntatulia

Oh my God is Better Sound



Credits
Writer(s): Lava Lava
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link