Kizunguzungu

Kwenye simu zimebaki picha na msg zako
Huwa napitapita kwenye page zako
Nasomaga sikufichi bado nina namba yako
Mwenzako namiss viemoji vya kopa kopa na vya kufumba macho
Huwa nakuona tu online unachat huishiwi bando n
Nitext tu niwe fine ziniondoke fikira mgando
Kwenye magroup ya whatsapp wee ndo bingwa wa
story tena kujibu upo sharp si wa nyuma nyuma toroli
Na ushapewa uadmin mset mipango
Aaaa
Riziki hapati mujini mshika michango
Aaaa
Hivi hunitaki kwanini au sina jambo
Namba yako kwa simu yangu imebaki pambo
Nifikiriie maana

Ooooh
Mwenzako hayaaniishi mawazo
Oooh
Najiuliza hivi nini chanzo
Ooohhh
Mwenzako hayaniishi mawazo
Ooooh
Najiuliza hivi nini chanzo
Mana kizunguzungu

Sijui nimwamini nani kwenye safari ya penzi langu
Nimkabidhi usukani akawe dereva wangu
Heeh
Mana majanga nalilia kisicho changu
Kwenye nyumba nilopanga nadai kodi wenzangu
Pakanja pakanja anavyochezesha moyo wangu
Akikohoa nabanja maradhi yake ndo yangu
Anapenda navyotabika na kusikitika ye anajimwaga tu
Machozi kububujika tu mi nadhalilika ananiona fyatu

Ooooh
Mwenzako hayaaniishi mawazo
Najiuliza hivi nini chanzo
Ooohhh
Mwenzako hayaniishi mawazo
Ooooh
Najiuliza hivi nini chanzo
Mana kizunguzungu
Naona kizunguzungu



Credits
Writer(s): Lava Lava
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link