Nitake Nini

Aaaaheeeh

Kwako tena sitamani
Nilishajua nilivaba
Huna jipya
Kurudi haiwezekani
Nishalioga janaba
Nikajisafisha mmmh

Oh maradhi yangu
Yamepata muuguzi
Mola wangu
Amenivusha vihunzi

Pole mwenzangu
Unokesha kwa waganguzi
Nishapata wangu
Anaejua nogesha chuzi

Naa ananipa mapenzi na kunijari dia
Ya nyuma niyasahau
Na anamaliza tenzi kutwa kunisifia
Kwa methali na nahau
Kwingine nitake nini

Ntang'angana, nang'ang'ania
Ohoo mimi
Nang'ang'ana nang'ang'ania
Sitaki madanga wa mjini

Nang'ang'ana, nang'ang'ania
Oohoo mimi
Nang'ang'ana nang'ang'ania
Aaah atake cha uvunguni

Sawa sawa
Pingili za sakafuni
Sawa sawa
Michezo ya kusaka kunguni
Sawa sawa
Tom na Jerry katuni
Sawa sawa (sawa)

Niliposema wa nini
Ye aliwaza atanipata lini
Kendembwe za nini
Na vijembe vya chini chini

Yupo makini
Penzi kashalibana na pini
Anipenda mimi
Hajazoea kuzini zini

Kwanza kakuzidi maarifa
Mpira tisini dakika
Nyavu anazitikisa aahee
Mlangoni mpaka kwa dirisha
Pindu ananipindisha
Mtoto ananifikisha aaaheee

Naa ananipa mapenzi na kunijari dia
Ya nyuma niyasahau
Naaa anamaliza
Tenzi kutwa kunisifia
Kwa methali na nahau
Kwingine nitake nini

Ntang'angana, nang'ang'ania
Ohoo mimi
Nang'ang'ana, nang'ang'ania
Sitaki madanga wa mjini
Nang'ang'ana, nang'ang'ania
Oohooo mimi
Nang'ang'ana, nang'ang'ania

Aaah atake cha uvunguni
Sawa sawa
Pingili za sakafuni
Sawa sawa

Michezo ya kusaka kunguni
Sawa sawa eee
Tom na Jerry katuni
Sawa sawa (sawa)



Credits
Writer(s): Lava Lava
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link