Woman Feat Victoria Kimani

Nilishatendwa sana
Nilishachekwa sana
Nilishakesha sana
Nikimlilia Maulana

Nilishategwa sana
N mitego ya wasichana
Nilishachimbiwa shimo
Wakiamini nitazama

Mi perfect kaumbwa mfano wa hasi na chanya
Na ju umeweza kusema amini nakupenda sana
Wengine majungu mtaji ndio maana wanachonga sana
Nimeumbwa kwa ajili yako
Wewe ni wangu tulia mama

Mpole, msikivu, mkweli, mvumilivu
Una mapenzi ya dhati kwenye shida mstahimilivu
Una malengo chanya, mcheshi na mwaminifu
Mahaba niteketeze chini juu sio mvivu

Unastahili tuzo
Tulia tule mbivu
Pokea hii nishani
Kawachome wenye wivu
My General, kwako nakiri mimi ni kurutu
Ninaweka silaha chini please... pokea saluti

Respect the woman
Protect the woman
Better love your woman
Woah mama, woah sister yeah

Where will I be without your love?
Oooh yeah
Where will I be without your love?

When am hungry you cook for me (ooh mama)
When am running you look for me (ooh sister)
When am hurting you hold on me (ooh mama)
Everyday you love on me, love on me
There I come for yah eeh

Respect the woman
Protect your woman
Love your woman
Oooh mama, oooh sister yeah

Unastahili heshima ya mizinga ishirini na moja
Uliniokoa sana nilipo onekana kioja
Tangu nimekuwa nawe umebadili maisha yangu
Kwenye shida na raha umekuwa karibu yangu

Kila nikiteleza umekuwa msaada kwangu
Kila mvua ikinyesha umekuwa mwamvuli wangu
Kila jua likiwaka umekuwa kivuli changu
Na kila kwenye majonzi umekuwa furaha yangu

Asante sana
Giza totoro we ndio kandili
Mungu tuongoze vyema pamoja tutunze family
Ni binadamu najua hatujakami-lika
Tumwombe Mungu tupatakapo tuta-fika

Sitokuacha kiangazi hata ma-sika
Iwake jua inyeshe mvua nita-fika
Nitaitika popote utakapo niita
Na mwisho nakuahidi kamwe sitobadi-lika

Respect the woman
Protect the woman
And love your woman
Woah mama, woah sister yeah

Where will I be without your love?
Oooh yeah
Where will I be without your love?

When am hungry you cook for me (ooh mama)
When am running you look for me (ooh sister)
When am hurting you hold on me (ooh mama)
Everyday you lover, you lover me

There I come for yah eeh
Respect the woman
Protect your woman
Love your woman
Oooh mama, oooh sister yeah

Tuna mengi tumeyavuka (ooh mama)
Mabonde kupanda mara kushuka (ooh mama)
Tumekata misitu jangwa na nyika (ooh mama)
Nimepita kote kwako najikita (ooh mama)

Where will I be without your love?
Oooh yeah
Where will I be without your love?

When am hungry you cook for me (ooh mama)
When am running you look for me (ooh sister)
When am hurting you hold on me (ooh mama)
Everyday you lover, you lover me
There I come for you



Credits
Writer(s): Joseph Haule
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link