Na Bado

Nimeamini bandu bandu,kweli humaliza gogo
We ni mfano wa chachandu,huwezi dandia mrago
Sikuwa kipofu wa mapenzi,kiasi unifiche tabia
Ulichofanya ni ushenzi,leo
Futa machozi kwanza kavute picha
Longtime ago ukiniita pacha
Ndoto yako mchana usiku kukucha
Leo mapenzi chakula ambacho
Si kwamba mimi nakusema kwa ubaya eee
I am sorry tena kama nimekosea
Usuthubutu kama kunizoea
Jifanye huna aibu mwisho watakuchea
Kama mfano ufananishwe na nani?
Mchano ukachanane na nani?
Mapenzi ukapendane na nani?
Wengine ni oversize, hatuendani

Mwanga niliwasha
Na kwonyesha upendo
Kipisijafanya zaidi ya vitendo
Moyo wako umeumiza moyo wangu ukaenda na bado nina wivu nakukumbuka ooh yeah

Kwa mdhaifu wa moyo,mpaka niogope mapigo
Sikukuvunja masikio,hadi ukanipa kisogo
Nilikuwa wazi,kama nyumba ya buibui
Leo unaleta uchizi, majanga mengi sijui
Wazazi unawakosea adabu
Heshima pia ustarabu
Unajiuza bila sababu
Nyumbani ushapajaza aibu
Hujali kuvishwa pete,bora kuvishwa mabwana
Huogopi giza tete,kila kiwanja unachana
Maboya wanakwita kimwana
Kumbe wanakuchora,namawenge kwasana
Nasikia siku hizi,unajiita mwali
Na hukumbuki hapo awali
Unatembea bila tahadhari
Ningekuwa boss ningekuongeza salary and Ferrari

Mwanga niliwasha
Na kwonyesha upendo
Kipisijafanya zaidi ya vitendo
Moyo wako umeumiza moyo wangu ukaendA na bado nina wivu nakukumbuka ooh yeah



Credits
Writer(s): Soso Jando
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link