Tajiri Yangu

Ewe, Ewe tajiri yangu
Wewe ndiwe kila kitu kwangu
Ewe, Ewe tajiri yangu

Wewe ndiwe kila kitu kwangu
We ni tajiri, wa matajiri
We ni tajiri, tajiri yangu

Lord, ni ngumu kujua we uko wapi ila unajua nilipo
Naiska haki kuipata ni bahati na kwa waganga siko
Vyuma vikiza najichangachanga kuusaka mshiko
Na mbanga zinakwaza madada wa kudanga wanabamba vifo

Na waliopinda we uwalinde no love
Ka wale wajinga walionipinga napowinda wokovu
Haunipi shida bila namna kuisolve
We ndio mmiliki wa kila tiba na hauna roho mbovu

Hauna roho mbovu unanipa incharge na power ninyanyue juu
Ni zaidi ya dawa sikuhitaji ninapougua tu
Unaniweka sawa devil akitua hamchukui Q
Una uwezo wa kunigawa au kuniumbua sio tu kuniumba mkuu

Ni rhumba tu ndio linaweka vumba juu na
Kututesa kama mfungwa anayechungwa kudundwa juu
We ndio BOSS ninaekuamini haututosi tukichomewa
Sio wale wanaowahi kazini ili wafoke tukichelewa

Ewe, Ewe tajiri yangu
Wewe ndiwe kila kitu kwangu
Ewe, Ewe tajiri yangu
Wewe ndiwe kila kitu kwangu
We ni tajiri, wa matajiri
We ni tajiri, tajiri yangu

Mwanadamu amemtawala mwanadamu kwa kumuumiza
Anakwapua mpaka asivyovihitaji bila kubakiza
Hii inafanya nafsi yangu ikose subira
Ikose usingizi, uoga huzuni niwe na hasira

Kwangu furaha nikiwa na MUNGU sio mlungula
Na pia siku zote mla raha na chungu hula
Najua nilipotoka,
Najua wapi nilipo isipokuwa ni we pekee unajua lini nitafika mwisho

Cheo chako ni kirefu zaidi ya dunia
Kipana zaidi ya bahari, ulinzi mkali hakuna askari anaefikia
Namlaani shetani kiundani nipate kujua mkuu
Ili nijihami na mtihani nisiache tusua Q

Najua una huruma naomba nikibuma usinitose
Mwanadamu atazingua heshima sio utumwa kwa Boss
Hauwezi nunua uhai sasa najidai kwa lipi?
Na kwako sote ... hata Malaya humpa ridhiki

Ewe, Ewe tajiri yangu
Wewe ndiwe kila kitu kwangu
Ewe, Ewe tajiri yangu
Wewe ndiwe kila kitu kwangu
We ni tajiri, wa matajiri
We ni tajiri, tajiri yangu

Siwezi kuwa masikini sababu
Anaenitunza ni tajiri ni MUNGU
Asieacha nigange njaa, nikose furaha, nikate tama

Ewe Ewe tajiri, yangu
We ni kila kitu kwangu
Umebeba uhai wangu
Umebeba maisha yangu
Tajiri wa uhai wangu
Tajiri wa maisha yangu
Tajiri wa kila kitu kwangu



Credits
Writer(s): Fareed Kubanda
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link