Shujaa

Yeee yeiyeeiii.
Tangu ulipokuwa msichana mdogo
Baba yako aliamini utafikia yako malengo
Niliamini hilo siku ya kwanza kukuona
Ukiwa umesimama
Pekeyako kwenye kona
Ulijawa ndoto
Nyingi kwenye macho yako
Ndoto zenye kuwasha moto unaofukuza machweo ya anga
Nilitaka kukushikilia
Sikuweza kukuzuia
Sababu akili yako
Umeilenga ambapo

Moyo wako unataka kwenda

Fata ndoto zako ntasimama nawe
Fanya unaloweza mi niko nawe
Ntakaa pembeni uniamini eyaa
Maana wewe unanipa nguvu
Mwanamke

Shujaa wangu
Shujaa wangu

Nakuona ni nyota
Inayong'ara
Ndani ya upeo wa macho yangu
Fungua macho ufate mwanga
Zikifunguka wingu
Nakuona una changamoto

Za kubadilisha ulimwengu
Tambua uwepo wako
Ukipigwa wimbi usipoteze lengo

Kokote unakotaka kwenda

Hakuna kukuzuia
Sababu akili yako
Umeilenga ambapo
Moyo wako unataka kwenda

Fata ndoto zako ntasimama nawe
Fanya unaloweza mi niko nawe

Ntakaa pembeni uniamini eyaa
Maana wewe unanipa nguvu
Mwanamke
Shujaa wangu
Shujaa wangu

Wewe ni shujaaaa
Usifadhaikeee
Usikate tamaaa
Usikate tamaaa
Usikate tamaaa eiyeee eeiiii
Shujaa wanguuu oooouuouuuu
Oooouuouuuu
Shujaaa wanguuu iyeeee...
Ooouwooouuuuuu
Shujaaa wanguu



Credits
Writer(s): Meltus Mujwahuzi
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link