Mama

Ooooh mama

Mama ninakupenda Mama
Mama ninakuheshimu Mama
(Mama eeh)
Mama ninakupenda Mama
Mama ninakuheshimu mama

Miezi tisa (eee ee)
Mbumbumbu sijui lolote
Ila Mama
Wewe waniongelesha
Miezi tisa (eee ee)
Tumboni sijui lolote
Ila Mama
Kabisa uliningojea

Ukashona na sare
Kusubiri nianze shule
Wakasema chizi yule
Si angengoja akuwe
Eeh, Mama siwezi kukulipa mimi
Uliyonipa hayanunuliki

Upendo wako mi sitosheki
Jembe, jembe Mama nakukubali wewe
Ooooh Mama

Mama ninakupenda Mama
(mama, mama--)
Mama ninakuheshimu Mama
Mama ninakupenda Mama
(Mama)
Mama ninakuheshimu Mama

Aah aah, ukitoa Mungu
Mbunge ni wewe ni wewe ni wewe
Waziri ni wewe ni wewe ni wewe
Raisi ni wewe ni wewe ni wewe Mama
Kila kitu ni wewe ni wewe ni wewe

Aah, nitanunua na kanga zenye maneno mazuri uone
Aaah tena nitazichanga na sarafu nikupe uchune
Aah, nitanunua na kanga zenye maneno mazuri uone
Aaah tena nikizichanga nitakupa na noti uone eeh Mama
Sijasahau sadaka zako kutoka moyoni
Uliponipa wakati Mama yangu hauna
Sijasahau sadaka zako kutoka moyoni Mama
Uliponipa Mama wakati wewe hauna

Tena kama nikienda Mama, jua ninakuthamini
Na moyoni mwangu nimekuweka Mama
Tena kama ukienda Mama, jua ninakuthamini
Na moyoni mwangu nimekuweka Mama

Oh kipenzi ooh kipenzi oh kipenzi oh
Oh mpenzi ooh mpenzi oh mpenzi oh

Oooh, Mama
Mama ninakupenda Mama
Mama ninakuheshimu Mama
Mama ninakupenda Mama
Mama ninakuheshimu Mama
Mama ninakupenda Mama
Mama ninakuheshimu Mama

(uuh)

Asante kwa malezi
Asante kwa vitumbua
Asante kwa chapati
Asante kwa kunikung'uta

Asante kwa malezi
Asante kwa vibajia
Asante kwa mandazi
Asante kwa kunipa bua

(Asante)



Credits
Writer(s): Goodluck Gozbert Wiki
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link