Shujaa

Aaah Tanzania, iye iye
Aaah Tanzania, iye iye
Aaah Tanzania (Selo beats)

Katika kila jambo
Unaloliona lapendeza
Jua kuna watu walioumia
(Kwa ajili hilo) Aaah (Kwa ajili hilo)

Katika kila jambo
Unaloliona lavutia
Jua kuna watu waliotaabikia
(Kwa ajili hilo) Aaah (Kwa ajili hilo)

Ni kweli Tanzania kuna amani ya kutosha
Hilo tunajivunia
Yatupasa tuliombee jeshi letu la taifa
Mola alotujalia

Wanapambana kwa ajili yetu oooh
Ili tuwe salama salama
Wanahangaika usiku na mchana oooh
Miili yao wametoa sadaka oooh

Wanalala kwenye vumbi na matope
Ili sisi tulale vitandani mwetu
Tunatembelea magari ya dhamani sana
Wanatembelea vifaru na malori

Asubuhi
Unaamshwa na alamu ya simu yako
Wao wanaamshwa
Kwa milio ya mabomu na risasi

Wanatoa sadaka yao leo
Kwa manufaa ya kesho yako
Wameyatoa sadaka ya maisha yao
Ili kutetea maisha yako

Twaiombea nchi yetu (Ooh Tanzania)
Nchi yetu (Ooh Tanzania)
Twaiombea jeshi letu (Mashujaa wetu)
Jeshi letu (Mashujaa wetu)

Twaiombea nchi yetu (Ooh Tanzania)
Nchi yetu (Ooh Tanzania)
Twaiombea jeshi letu (Mashujaa wetu)
Jeshi letu (Mashujaa wetu)

Unavaa mkanja mzuri kiuoni mwako eeh
Wanavaa mikanja ya risasi.ii.ii... ii
Unakula chakula ukipendacho, kile ukitamanicho
Wanakula wadudu na matunda porini (porini)

Tunavaa kofia maridadi
Na nzuri zenye kupendeza
Wanavaa kofia ngumu
Na nzito tena za chuma

Sijutii kuzaliwa Tanzania
(Aah...)
Najivunia mimi kuwa Tanzania
(Aah...)

Wanapambana kwa ajili yetu oooh
Ili tuwe salama salama
Wanahangaika usiku na mchana oooh
Miili yao wametoa sadaka oooh

Asubuhi
Unaamshwa na alamu ya simu yako
Wao wanaamshwa
Kwa milio ya mabomu na risasi

Wanatoa sadaka yao leo
Kwa manufaa ya kesho yako
Wameyatoa sadaka ya maisha yao
Ili kutetea maisha yako

Twaiombea nchi yetu (Ooh Tanzania)
Nchi yetu (Ooh Tanzania)
Twaiombea jeshi letu (Mashujaa wetu)
Jeshi letu (Mashujaa wetu)

Twaiombea nchi yetu (Ooh Tanzania)
Nchi yetu (Ooh Tanzania)
Twaiombea jeshi letu (Mashujaa wetu)
Jeshi letu (Mashujaa wetu)

Twaiombea nchi yetu (Ooh Tanzania)
Nchi yetu (Ooh Tanzania)
Twaiombea jeshi letu (Mashujaa wetu)
Jeshi letu (Mashujaa wetu)

Twaiombea nchi yetu (Ooh Tanzania)
Nchi yetu (Ooh Tanzania)
Twaiombea jeshi letu (Mashujaa wetu)
Jeshi letu (Mashujaa wetu)



Credits
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link