Bado

Kutwa kidomo wazi, nikifuta na machozi
Huku namuomba Mola unitoke moyoni
Ila ndo siwezi, nakesha ka mlinzi
Maana hata nkilala unaniijia ndotoni

Lato, asante kwa kuniumiza
Nimejifunza mengi, mwanzo sikuyajua
Katu, naapa kutolipiza
Ila mwambie mapenzi abaki kuyasikia, eeeh

Nakumbuka maneno yako
Hutonikimbia, utabaki nami
Tena ukala na viapo, Taurat, Bibilia

Leo sikuoni, ila mwenzako bado
(Bado bado, bado bado)
Mwambie bado
(Bado bado, sijapona)

Ila mwenzako bado
(Bado bado, bado bado)
Mmh bado
(Bado bado, sijapona)

Misijapona roho
Aa-ah Mola nishike mkono Baba Muumba
Haya ninayoyaona, simanzi
Ah, yaani bora jicho mchanga ningefumba

Huenda ningeshapona, maradhi
Oh maumivu yangu, hayawezi kupona kwa vidonge
Sababu panaponichoma, nikipapasa sipaoni
Kweli peke yangu, umeniacha na unyonge

Kabisa wakanipokonya tonge langu mdomoni
Ona, nakumbuka maneno yako
Hutonikimbia, utabaki nami
Oh, mi ndo mwili, mi roho yako
Yaani umetimia, mbona sikuoni

Ila mwenzako mimi
(Bado bado, bado bado)
Mmh, nambie
(Bado bado, sijapona)

Ila mwenzako bado
(Bado bado, bado bado)
Mmh bado
(Bado bado, sijapona)

Ile roho yangu mama
(Ibebe)
Inandondoka
(Ibebe)
Iokote mama
(Ibebe, Chaukucha nsije zima)

Uh roho yangu
(Ibebe)
Inandondoka
(Ibebe)
Njoo unshike mama
(Ibebe, Chaukucha nsije zima)

Ah aah, ai wewe
(Ibebe)
Watanizika mama
(Ibebe)
Mwenzio taabani
(Ibebe, Chaukucha nsije zima)

Masikini pendo langu
(Ibebe)
Linandondoka
(Ibebe)
Niokote mama
(Ibebe, Chaukucha nsije zima)

Ibebe, ibebe
Ibebe, Chaukucha nsije zima
Ibebe, ibebe
Ibebe, Chaukucha nsije zima



Credits
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link