Ongeza

Mhhh, mhhhh
Mi kwako sikuingia miguu
Mikono hadi kichwa kiufupi mazima
Nikiamini wa kufa kuzikana
Yani hoi isio nafuu
Maututi kabisa hata mashaka siiina
Nikiaminiiii tutatengwa na Maulana
Mvumilivu hula mbivu
Nimengoja mpaka zikaoza
Naambulia maumivu
Ingali sina wa kupoza
Sijui yangu stahamilivu kumnyenyekea kwaniponza
Napambania utulivu mwenzangu chuki unaikoza

Sikukufuta tu machozi ulipolia nililia na wewe
Sa mbona wanilipa majonzi
Yani stress mapombe nilewe
We ndo wangu Yesu Mkombozi
Sa mbona Petro unaniacha mwenyewe
Nikose usingizi na njozi ndo ufurahi
Ok sawa si unataka nitukanwe

Ongeza, ongeza badooo
(Nidhalilike)
Ongeza, ongeza badooo
(Nikose pa kuificha sura)
Ongeza, ongeza badooo (marafiki wanicheke)
(Waning'ong'e hadaa)
Ongeza, ongeza badooo

Mmmhh kisichokuua hukukomaza eti kiuskali huo msemo mi nakataa
Mana jua linapoangaza ndo sina afadhali mie kwangu ni mabalaa
Oooohh najitahidi kumsinga mwali ila somo ananikataa
Ooohhh penzi letu si la kibatari anayamwaga mafuta ya taa
Kutwa ni vurugu ndani
Purukushani hapakaliki
Roho inaniuma yani kwa nini sa tunagombana sweet
Ooohh jema gani nambie labda nitende kipi
Hata pa kucheka honey eti utani unapaniki
Naelewa ridhiki mafungu saba na la kwangu sita
Naelewa sikutoshi labda kukuridhisha
Sikukufuta tu machozi ulipolia nililia na wewe
Sa mbona wanilipa majonzi yani stress mapombe nilewe
We ndo wangu Yesu Mkombozi
Sa mbona Petro unaniacha mwenyewe
Nikose usingizi na njozi ndo ufurahi
Ok sawa si unataka nitukanwe

Ongeza (eheeeee), ongeza badooo (eheeeeee)
(Nidhalilike)
Ongeza, ongeza badooo(eee)
(Nikose pa kuificha sura)
Ongeza, ongeza badooo
(Ndugu jamaa wanicheke, waning'ong'e hadaa!)
Ongeza, ongeza badooo (ehee)
Nikose pa kuificha sura
Ah, waning'ong'e hadaa...



Credits
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link