Haunisumbui

Si kokoko si kandambili, yani vyote havikupendezi
Mwana ngoko usionawili, tope bin uterezi
Utaishia kututabiri tubomoke, inasonga miezi
Mola amesha takabiri, usijichoshe livunjiki penzi
Ona! Umekosa nuru, umekosa bahati huna
Unaitwa kunguru, ukifika wananuna
Ndondondo mwana chururu, asie buzi wataka chuna
Mengine nisikufuru

Hhmm! Hazikukai maskara, wala makeup zinakushuka
Uso umekuparara, mwili shockup zimetenguka
Uso, sauti ya Stara, pakudeka unawehuka
Jibwa koko la Mbagala, unabweka na kubwetuka wala!

Wala haunisumbui wala!
Wala haunisumbui wala!
Wala haunisumbui wala!
Wala haunisumbui wala!

Na izo post, mara kubebana, mara eti mnabusu mtamaliza bando
Unaowatuma kunitukana, siogopi mashushu mi wala michambo
Kutwa kwa ma-page feki kama Lokole inahusu?
Mkwe akutaki eti mwenzangu pole mbona kuntu
Vimeseji kujitumisha kwa ndugu zangu marufuku
Nyota imekufubika, usifosi umaarufu
Upepo wa kisulisuli, umekuchukua na nuksani
Tanga Lipulipuli, wanakununua kwa mizani
Kwangu pambe shughuli, najiashua burudani
Nna toto zurizuri, nimelitua tuli ndani yi yi yi hi
Umekosa nuru, umekosa bahati huna
Unaitwa kunguru, ukifika wananuna
Ndondondo mwana chururu, asie buzi wataka chuna
Menginе nisikufuru, usie wa Shaba wala Chuma

Wala haunisumbui wala!
(Hamunikondeshi)
Wala haunisumbui wala!
(Mujipost mainstagram)
Wala haunisumbui wala!
(Hamunitetеreshi)
Wala haunisumbui wala!
(Waalaah)

(Waasafi)



Credits
Writer(s): Siraju Amani
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link