Sikomi

Wanasemaga mapenzi safari, unavyopita ndo jinsi unajongea
Ila niendako ni mbali sijui ka ntafika sababu natembea
Niliposikiaga habari, yakisifika nikakesha nangojea
Akabariki Jalali na nikawika muziki nikauotea
Ile pruuu mpaka Macca nikadandiaga Bongo movie
Kumbe mapenzi hayataki haraka, ni kama tango natia tu chumvi
Mwenzenu nikaoza haswa, na kujitia kitandani mjuzi
Eti nataka fukuza paka, badala ya mbwa nikafuga mbuzi

Hhhmmm
Wivu ukanifanya nikagombana na marafiki
Ugomvi na mamangu akiniambia siambiliki

Moyo ukanambia Nasibu sasa mapenzi basi
Ila nang'ang'ania najaribu kuipinga nafsi
Esma ananiambia mdogo wangu mapenzi basi
Ila nang'ang'ania
Nikiumizwa na huyu kesho nna mwingine

Ooh mbona sikomi
Sikomiii
Sikomi
Licha ya mateso haya
Najiuliza (oh sikomiii)
Oh sikomi mbona (sikomiii)
Mbona jamani
Sikomi
Licha ya mateso haya
Hhhhmmm

Aliyonifanyia wa central
Haki ya Mungu siyawezi sema
Ila nimejifunza kesho nisiwaamini wacheza sinema
Moyo walinipatia mateso
Siwezi kumeza siwezi tema
Ndio maana sikushanga ile ghafla
Toka CCM kwenda CHADEMA
Wanasema kitanda ukitandika sharti ukilalie
Nikajitia ukamanda yatakwisha
Wacha nivumilie
Kila kiza kikitanda
Ndo visa machozi me nilie
Penzi yakatia parapanda
Kuwaita waje washambulie
Aah
Acha na Penny we darling
Nilio muhongaga gari aliponambia ana mimba mwisho wa siku akaichomoa chaliiiii
Mola akanitunuku Zari akanzalia dume na mwali
Niliyvo mjinga nikacheat aibu mpaka
Kwa vyombo vya habari

Moyo unanambia Nasibu sasa mapenzi basi
Ila nang'ang'ania najaribu kuipinga nafsi
Lizer ananiambia Simba mapenzi basi
Ila nang'ang'ania
Nikiumizwa na huyu kesho nna mwingine

Ooh mbona sikomi (mboooona)
Sikomiii (mbona jamani)
Sikomi
Licha ya mateso haya
Eh nishafumania (oh sikomiii)
Nikafumaniwa mimi (sikomi)
Nishagombana na watu (sikomiii)
Licha ya mateso haya (mateso haya)



Credits
Writer(s): Inconnu Compositeur Auteur, Solly Cohen
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link