Pastor

Yeah!
Wacheni watoto wadogo waje kwangu
Maana ufalme wa Mbinguni ni wao
J. Rider where you are
I'm the pastor of this church
I'm the pastor of this church
I'm the-, it's Tongwe Records

Fanya ishara ya msalaba, upokee haya mahubiri
Mimi ni mteule, ninawaletea injili
Nina ushuhuda wa kiroho, Bwana yuaja msubiri
Natangaza upako, na habari za mnara wa Babeli

Wachungaji wanalumbana wakigombania waumini
Wanalala (wanalala), wakiamka wanaanzisha dini
Hawaogopi damu ya msalaba, Bible wanaifanya biashara
We siyo Yesu hatakama baba yako fundi seremala

We' ni nani usokosea kila unayemuombea anapona?
Hatutaki shuda za uongo, aminini nyote mtachomwa
Ndani ya vazi la suti, unakebehi wakatoliki
Mtaleta dini zote ila R.C itabaki

Hata Kristo alipoponya hakutaka malipo
Account yako imejaa sadaka zetu wakristo
Toba yako haijaswihi halafu unajiita una upako
Sio kila ata'yenita bwana basi ataiona pepo

We' ni nani unayejiita nabii kwenye jamii?
Hizi nyakati za mwisho, soon atashuka Masihi
Piga magoti tusali (amen)
Piga magoti tusali (amen)

Waumini wamekimbia kanisa, madhehebu yanaongezeka
Hizi nyakati za mwisho, check manabii wa uongo!
Mwana wa Adam yuaja (amen)
Mwana wa Adam yuaja (amen)

Laiti ningeweza, ningekugeuza jiwe la chumvi
Vipi unipangie sadaka? Pastor gani? We mlanguzi
Hakika ili neno, "Usitumikie mabwana wawili"
Siasa na kanisa kama hadithi za Cain na Abel

Ka' wasabato was'okula kitimoto wala kambare
Wanasadiki mbele ya haki, wanaamini agano la kale
Mnatangaza ufahari wenu kwenye vikapu cha sadaka
Hakuna sadaka ya kweli kama kumchinja Isaka

Kanisa lako halifanani na ufalme wa Jehova
Madhehebu yanajitenga kama makundi ya bongo fleva
Heshima ya mkatoliki, inashuka kama theluji
Dini mmeifanya miradi kwa kivuli cha uchungaji

Kanisani mnaonyeshana, ufahali wa kuvaa bazeee
Hekalu mnalichafua kwa sadaka ya pedeshee
Biblia hujaimaliza unataka uzima wa milele
Usije ukatuchoma moto ka' wafuasi wa Kibwetele

We' ni nani unayejiita nabii kwenye jamii?
Hizi nyakati za mwisho, soon atashuka Masihi
Piga magoti tusali (amen)
Piga magoti tusali (amen)

Waumini wamekimbia kanisa, madhehebu yanaongezeka
Hizi nyakati za mwisho, check manabii wa uongo!
Mwana wa Adam yuaja (amen)
Mwana wa Adam yuaja (amen)

Hizi nyakati za mwisho, soon atashuka Masihi
Wewe una mamlaka gani mpaka unajiita nabii
Kukataza waumini wasivae mapambo kwako jadi
Ili pesa wakupe sadaka na kisha unafanya mtaji

We' mchungaji umekusanya waumini kwenye vijiji
Ukawaongoza sala ya toba kama Yohanna mbatizaji
Unabeba gunia la zambi, na Yesu kumvika taji
Usini'ekee mkono kichwani huna karama ya uponyaji

Imani yako ndogo kama punje ya aradani
Uza mali zako zote pesa uwape maskini
Si unatupa kiini macho unatumia gari ya kanisa
Halelluya halelluya, kumbe unatuibia sadaka

Yesu hakuwa mganga wa kienyeji japo alimponya kipofu
Kwa tope la mate yake ila kwako napata hofu
Eeh, Mungu napiga goti hiki kikombe kiniepuke
Mwana wa adamu yuaja basi tungoje ashuke

We' ni nani unayejiita nabii kwenye jamii?
Hizi nyakati za mwisho, soon atashuka Masihi
Piga magoti tusali (amen)
Piga magoti tusali (amen)

Waumini wamekimbia kanisa, madhehebu yanaongezeka
Hizi nyakati za mwisho, check manabii wa uongo
Mwana wa Adam yuaja (amen)
Mwana wa Adam yuaja (amen)

"Angalieni mtu asiwadanganye
Maana wengi watakuja kwa jina langu wakisema mimi ni Kristo
Nao watadanganya wengi", halellujah (ameen)
"Manabii wengi wa uwongo watatokea
Kutakuwa na dhiki kubwa siku hiyo
Je hamsadiki ya kuwa hizi ni ishara kwamba mwana wa adam yuaja?" (Amen)
"Basi kesheni mkisali maana hamjui saa wala siku"

I'm the pastor of this church
I'm the pastor of this church
I'm the-, it's Tongwe Records



Credits
Writer(s): Ibrahim Musa
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link