Mr. President

By... Mwl. Julius Kambarage Nyerere
Ikulu ni mahali patakatifu, ikulu ni mahala patakatifu
Mimi sikucha guliwa na wananchi wa Tanzania
Kuja kupageuza kuwa pango la walanguzi
Claps claps claps
By... Roma
Drop drop drop drop drop yop
Haaa haaa... yes Surprise ...Tongwe records
We are here for revolution wooord
Mr. president .welcome to white house
Thank you... aaaah ...thank you ...yeaaah
Mi ndo' roma mkatoliki mwenye asili ya kiyahudi
Mpare wa milimani sa lamu ya kikwetu urewedi
We ni mkwere wa chalinze ambaye hutamsahau mnyakyusa...(Mwakyembeee)
Aliye wafundisha monduli siasa
Aliyekula kiapo kwa agano jipya la wakorintho
Siyo msabato mwenye siasa za kubattle kama Zitto
Mwenye wito wa Appocalypto husssle za Kambikatoto
Msaka ndoto kama kristo shujaa kama Mrisho Mpoto
Jasiri kama Mandela busara kama Nyerere
Niliyejificha mapangoni mithili ya Otango Osale
So usinidanganye kwa uchawi waaa kutumia ndulele
Au vita vya majimaji nife kama Kinjekitile
Hatutaki siasa za kale, siku hizi tunawahi kubalehe
Nawapa pole wakazi wote wa Tandale kwa Mtogole
Akhsante Sheikh umeniita ikulu sio kisa nina nyota ya mshale
Najua mvi sio busara ila naomba amani itawale
Ikulu yako ina thamani zaidi ya falme za kiarabu
Cha ajabu hawaithamini na inapoteza thawabu
Taifa lilikutabri tangu enzi ukiwa waziri
J.K wa 2 utakuja ongoza hii serikali
Yenye vilio kote kama kina mama wa Galilaya
Wanaoutafuta ukombozi wasimamishe Pobilahaya
Viongozi wetu ni mafia na mabeautifull lier
Nilikuwa na ndoto hizo ila bado hawaja niinspire
Angalau mapinduzi kama Macio Maximo
Usihangaike kumtafuta Roma... mi!! Hakimu wa getho
Mwenye sauti ya mamlaka!!! iliyomfikisha Mrombo Keko
Baada ya kukemea ufisadi na sera za Karamagi
Na waliokula jasho letu kwenye migodi ya Buzwagi
Utazuia vipi ongezeko la wimbi la ukeketaji...
Wakati Ngariba ndo' diwani wa kata kwenye kijiji!!
Neither do I...!! hongera ulipima ukimwi
Watanzania nasi tuamke tusimpige kibao tu Mwinyi
Hapa nagundua aya-tul - munafik - thalatha
Inawezekana aliishia alifu wakati anasoma madrasa
Huu sio muda wa kujadili kesi za Manji na Mengi
Hayo ya Mungu we Kaisari jadili mambo ya msingi
Teacher alipojiita mtabiri Tanganyika wote vipofu
Padre wa kwanza pentekoste ubatizo wa maji marefu
Machozi yalinitoka Segera watoto hawapati haki
Wengi wamekimbia shule basi lije wauze visheti
Wanaosomeshwa kwa mtaji wa chapati na uvuvi wa samaki
Wabunge wao wamekaa na wanajiita wanaharakati!!
Rudi kwenu kahamasishe nduguzo hawana taaluma
Wazaramo wamegoma soma still mwali wanamcheza ngoma
Wanalia Kilwa Kivinje huku wanaocheka ni wabunge
Walionunua kura ya bibi kwa kumuhonga doti ya kitenge
Hata wamasai walikuchagua kwa kura nyingi za upendo
Wakiamini mtetezi yuaja wa jimbo la Oldoyo Sambo
Waambie what is going on ndani ya himaya ya bwawa la Mtera
Waonyeshe na mikataba ya utawala wa mgodi wa Kiwira
Jeshi lote kwenda Tarime hawakuwa na njia mbadala
Na walioteketea Mbagala!!
Mr.pres ... Haya masikharaaaa!!!
Sina maana utoke wewe hicho kiti umuachie professor
Nisamehe kama nakosea maana mimi sio mwanasiasa
Claps claps claps
By... Mwl... Julius Kambarage Nyerere
Kwa hiyo kitu kimoja tunataka kuelewa...
Ni hali ya matatizo ya nchi yetu yalivyo sasa hivi... Eee!!
Kwasababu... sera ya... ay... awamu ya kwanza... awamu yangu mimi...
Imefanya mema... imefanya ya kijinga...
Ya kijinga yanaachwa...!! lazima yaachwe...
Ubaya wenu ni kwamba... mnaacha mema... mnachukua ya kijinga



Credits
Writer(s): Ibrahim Musa
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link