Nimwage Radhi

(Harmonize)
furaha isio kifani kukupata
mwandani hakika wamependeza
goma lipo uwanjani kaibiwa nani
sa unaachaje kucheza

(mpoto)
ama kweli harusi imefana tena ya ki historia
pande zote baba na mama naona
wanashangilia ila sitaki kua
mnafiki jumba bovu kuniangukia
nina langu moyoni
ningependa kuwaambia

bi harusi mashoga wa kukupia hao
ni wa kuwaangalia
wako wale u hali gani
wanakuja kuchungulia owaombe
samahani uwakomeshe wambea
eti wifi umepika nini na mimi utanigaia waambie
umepika dagaa zenye pili pili nyingi
zinakutosha wewe na na mme wako
wao watakimbia

(harmonize)
eeh aiii shemeji tubu ya mmeo
usikize ya fulani na hii ndo meseji
sema na mmeo usitafute ya jirani
kwa furaha niliyo nayo niacheni
nimwage radhi aiyoyoo
niacheni nimwage
radhi mi nataka nimwage radhi

(mpoto)
ng'ombe anapoita ndama tunasema
kwamba analia kupigwa na kulalama
hatujawahi kusikia hakika mmpendeza mi
navyomfahamu bi harusi
sipati kusimulia nimetokea
ruvuma chogolo,namtumbo lindi
mtwara mpaka chatoholi nimezisikia

(mpoto)
sifa binti huyu mola amemjalia
binti hapendi majungu hakika ni
nachowaambia ukimuazima viatu
na gauni anakuachia bwana harusi
tunakupa mke ukaishi naye vyema
nyumbani huna kitu husimfiche
mwambie tahadhari

(mpoto)
ikiwezekana mkakope mkono uende
kinywani husimpige mateke kisingizio
kitu fulani ohh umefanya nini
jana hakuliki mtoto bado mteke
usimkomaze kwa ngumi
ukishindwa mrudishe kwao hajaua huyu

(mpoto)
mmeo akienda kazini akirudi
salimia wala husikae chini chakula
kumsukumia mkaribishe ndani
hali ukimjulia muulize za kazini
kwa tabasamu muruaa
kisha msindikize bafuni ata kama anapajua
alafu wewe tafuta kiti jikoni kimbilia
simu yako meseji ukimtumia mwambie
bila wewe chakula hakitaingia

(harmonize)
eeh aiii shemeji tubu ya mmeo
usikize ya fulani na hii ndo meseji
sema na mmeo usitafute ya jirani
kwa furaha niliyo nayo niacheni
nimwage radhi aiyoyoo
niacheni nimwage
radhi mi nataka nimwage radhi

(mpoto)
nawaomba niishie hapaa taarishi
hua hafungwi naomba nichape lapa
yaliyobaki ni ya makungwi
niliowakera samhani kusema ni jukumu
langu nawaomba muishi kwa amani
hio ndio furaha yangu

(harmonize)
mmmh
ndoa ni kama safari
tuombeane dua atuepushe na shari
sa chini ya jua aah somo yake
mwari ainuke mama yake mwari
ainuke baba yake mwari ainuke
aje kati tulicheze ngoma kaka
yake mwari ainuke dada yake mwari
ainuke shangazi yake mwari ainuke
aje kati tulicheze ngoma

(harmonize)
niacheni nimwage radhi
mi nataka nimwage radhi
niacheni nimwage radhi
niacheni nimwage radhi
mi nataka nimwage radhi



Credits
Writer(s): Siraju Amani, Rajabu Kahali, Mrisho Mpoto
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link