Baba

Tongo Records

Binladen

Ah, kwanza naomba ukaechini
Alafu uvute pumzi
Nna vitu vya kuongea, ambavyo unajua vita kuudhi

Ivi unajua nimekuvumilia sana
Angekuwa mtoto mwingine tayari ungeishampa laana
Najiuliza sijui nikuseme na kipi baba
Najuiliza sijui nianze na lipi labda

Mama anasema, mwanzo mimba uliikataa
Kwani sasa hukutoa, ukaruhusu mpaka akazaa?
Alafu, hivi auzijui kinga?
Au hukujua peku peku kama italeta mimba

Uchi wako wa kijinga ndo sa'ivi unanitesa
Usinge mrubuni mama labda angemuoa barkhersa
Dah! Unanipata kiwewe, au manesi walichanganya
Baba angu hakuwa ni wewe!

Kama unataka kunipiga, leo yote sawa
Au nikuchumie fimbo unichape kisawa sawa

Hata kama ni mzazi
Saa zingine nawaza nikuchukie
Sema tu we ni mzazi
Acha ukweli wako nikuambieee

Daddeeey olaaa!
Naongea na weweee e
Daddeeeeey
Naongea na wewe naongea na wewe!

Ile hela ya kuonga ungeitoa ka sadaka
Mungu ange kubariki ungenizaa kasadaka
Ukajichanganya Kaisari ukampa isiaka

Alafu mbele ya yesu petro ukampa mamlaka

Mbona mzee mushi, namuona na hela
Mzee mwakalinga, mwenzie anahela
Mzee lutashobwa ndo kabisa ana mielea

Wewe ulikuwa wapi mpaka unakofa kabwela
Nikuulize, ukifa nitarithi nini, labda jina laukoo
Alafu linisaidie nini?

Utajiri hivi hukuuona kwanini
Maana pombe unazo kunywa, siwezi rithi hadi maini
Umeshindwa hata kununua kiwanja?!
Ona mpaka leo tupo nyumba za kupanga

Elimu sikuizi nibure, ila cha ajabu umeshindwa hata kunipeleka shule!
Inauma sana, ila acha tu nikuulize
Inama ujana wako umeshindwa kuwa bize?

Nikiendelea kuongea naona kama nitakufuru
Nimemaliza, nakuombea kwa mungu akupe nuru!

Hata kama ni mzazi
Saa zingine nawaza nikuchukie
Sema tu we ni mzazi
Acha ukweli wako nikuambieee

Daddeeey!
Naongea na weweee e
Daddeeeeey
Naongea na wewe naongea na wewe!

Mwanangu nimekusikia nakuombea kua uyaone
Nilijua umekuja kwangu kuniombea ili nipone
Kumbe umekuja kwa shari, kunilaumu, nakuniukumu

Inaonyesha ningesinzia ungeninywesha hata sumu!
Baada ya ujauzito wako tulipima na mama ako
D.N.A ilionyesha kuwa mimi sio damu yako

Ukisikia ukuwbwa jalala, basi juwa dunia dumple
Nikasimama kivie kupigania maisha yako

Tena nilingoja ngoja ukuwe
Nikajitoa kwa hali na mali ili usijue
Nikafanya mambo mengi ya atari ili nikutunze
Waka nisweka jela ili dunia inifunze

Ukuaji wako, sidhani ulilishwa mila
Nilipambana kilakona kuwa tafutia ngawila
Niliuza mali zangu ilimradi wewe usome

Leo unanipandishia kibezi, nyambazu tena unikome!

Muone mtoto wa sobo, mwenzio ni rubani
Mtoto wa sugu juzi kapa ud1
Mtoto wa bwile ndo doktari marekani

Ebu toa bangi zako, aliekuambia usisome nani?!

Hata kama ni mzazi
Saa zingine nawaza nikuchukie
Sema tu we ni mzazi
Acha ukweli wako nikuambieee

Daddeeey!
Naongea na weweee e
Daddeeeeey
Naongea na wewe naongea na wewe!

Hata kama ni mzazi
Saa zingine nawaza nikuchukie
Sema tu we ni mzazi
Acha ukweli wako nikuambieee

Daddeeey!

Elimu sikuizi nibure, ila cha ajabu umeshindwa hata kunipeleka shule!

Daddeeey!

Ebu toa bangi zako, aliekuambia usisome nani?!

Tongo Records

Binladen



Credits
Writer(s): Haule Joseph, Stamina Shorwe Bwenzi
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link