Ningefanyaje

Sio siri mama, nilikujali sana
Na kujiheshimu
Nilijua kwamba, Mungu akipenda
Nitakuwa nawe
Usidhani kwamba, nilikusudia
Kutengana nawe
Mi sijui, hapa nilipo saa hii
Nimefika vipi

Alivyoniingia (sikumbuki)
Akanizoea (sikumbuki)
Moyo akanipa, na wangu nikautua
Alivyoniingia (sikumbuki)
Akanizoea (sikumbuki)
Moyo akanipa, na wangu nikautua

Ningefanyaje, na we, haukuwa karibu na mimi
Lakini ye, ndiye, aliyekuwa ananijali mimi
Nitafanyaje, na ye, yu tayari kuishi na mimi
Lakini we, ndiwe, tulizo la moyo wangu mimi

Sio siri baba, nilikupenda sana
Na kukuthamini
Nikiamini kwamba, Mungu akipenda
Nitakuwa wako
Mi najua kwamba, umekusudia
Kutengana nami
Na mi sijui, hapa tulipo oh oh
Tunatoka vipi

Alivyoniingia (sikumbuki)
Akanizoea (sikumbuki)
Moyo akanipa (na wangu nikautua)
Alivyoniingia (sikumbuki)
Akanizoea (sikumbuki)
Moyo akanipa (na wangu nikautua)

Ningefanyaje, na we, haukuwa karibu na mimi
Lakini ye, ndiye, aliyekuwa ananijali mimi
Nitafanyaje, na ye, yu tayari kuishi na mimi
Lakini we, ndiwe, tulizo la moyo wangu mimi

Ningefanyaje, na we, haukuwa karibu na mimi
Lakini ye, ndiye, aliyekuwa ananijali mimi
Nitafanyaje, na ye, yu tayari kuishi na mimi
Lakini we, ndiwe, tulizo la moyo wangu mimi

Ningefanyaje, na we, haukuwa karibu na mimi
Lakini ye, ndiye, aliyekuwa akinijali mimi
Nitafanyaje, na ye, yu tayari kuishi na mimi
Lakini we, ndiwe, tulizo la moyo wangu mimi

Ningefanyaje? (oh aya yaya)
Ningefanyaje? (oh aya ya)
Ningefanyaje? (oh aya yaya)
Ningefanyaje? (oh aya yaya)
Ningefanyaje? (oh aya ya)
Ningefanyaje? (oh aya yaya)

Credits
Writer(s): Avril Nyambura Mwangi
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link