Kwa Ajili Yako

Najua hiki ndio kipindi ukipendacho
Najua sasa hivi uko karibu na redio
Labda peke yako hauna rafiki zako
Naomba kidogo ongeza sauti ya redio

Nachukua nafasi kuongea nawe kwa wimbo
Nimetunga special kwa ajili yako mrembo
Mtangazi kati ya wimbo usiweke jingo
Nimetunga rasmi kwa mtu aliye single

Kwa ajili yako naimba
Sauti hii sikia
Habari hii pokea
Zingatia mrembo
Usiguze mrembo
Zingatia mrembo
Usiguze mrembo
Zingatia
Zingatia... ah ah

Ndani ya roho yangu uko peke yako
Usihofu mami hakuna mwenzako
Nimezaliwa mimi kwa ajili yako
Ninaahidi sitotupa penzi lako
Nimekupa nafasi kubwa ndani ya moyo
Fursa tu uniite baba watoto wako
Kipingamizi hakuna juu yako
Come closer nipunguze mapigo ya moyo

Kwa ajili yako naimba
Sauti hii sikia
Habari hii pokea
Zingatia mrembo
Usiguze mrembo
Zingatia mrembo
Usiguze mrembo
Zingatia
Zingatia... ah ah

Moyo wangu unatamani sana
Mimi kuwa na wewe
Wacha niseme hadharani
Kila mtu asikie
Moyo wangu unatamani sana
Mimi kuwa na wewe
Wacha niseme hadharani
Kila mtu asikie
Asali ni tamu baby
Kwa wanaoifahamu
Ila ni chungu sana, kwa wasioifahamu
Songea karibu yangu yangu, tulia kabisa
Lala kifuani mwangu,sinzia kabisa

Kwa ajili yako naimba
Sauti hii sikia
Habari hii pokea
Zingatia mrembo
Usiguze mrembo
Zingatia mrembo
Usiguze mrembo
Zingatia
Zingatia... ah ah
Zingatia
Zingatia
Zingatia



Credits
Writer(s): Hussein Juma
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link