Na We Upo

Siioni furaha pale nilipo
Usoni karaha mahangaiko
Tumefunzwa kupiga, upendo hakuna, mradi kupata
Tunatafuta faida, rushwa ndo sana, utu tumekataa
Ujanja kupata, bila kujali nani amekosa
Tumejaa utata, wizi ndo dili, heshima imetoswa
Ulipo moyo wako huo, hazina yako hiyo
Na we upo
Ulivyo upendo wako huo, utu wako huo
Na ye yupo
Ukibadili moyo wako huo, hazina yako hiyo
Na we upo
Ukiongeza upendo wako huo, utu wako huo
Na ye yupo
...
Izzy naomba mic bruh
Tusome, tusome (Mkulima)
Tunataka wana, tunataka wana kwa kitaa ah
Masela wana, mamanzi wana kwa kitaa ah
Yeah
Tunakula nao, maisha twafanya nao
Kijiweni tuko nao (yeah) na stori ni zao
Maisha yao, dili zao, vyote vyawasuta wao
Matendo yao ya chuki na hawaendani na maneno yao
Kipi twapata na, nini twafanya bruh
Show love show love, sikia wakikukanya
Maisha kwa wote balaa, kote karaha
Hauko pekee mwenye njaa
Usione masela wako bar, wana furaha
Ukaona life yako kinyaa
Umechagua kuishi hivi, weka bidii
Sio kutwa kwa TV
Furaha uchaguzi, jali jamii
Jirani ni ndugu chalii
Ulipo moyo wako huo, hazina yako hiyo
Na we upo
Ulivyo upendo wako huo, utu wako huo
Na ye yupo
Ukibadili moyo wako huo, hazina yako hiyo
Na we upo
Ukiongeza upendo wako huo, utu wako huo
Na ye yupo
Tunataka wana, tunataka wana kwa kitaa ah
Masela wana, mamanzi wana kwa kitaa ah
Yeah, ya Mungu mengi ujue
Wewe shukuru tu, always



Credits
Writer(s): Bonus Ansgar Lwiwa
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link