Mama

Nani kama mama?
Katika hii Dunia
Kwa mapenzi na huruma
Mfano hajatokea

Nani kama mama?
Katika hii Dunia
Kwa mapenzi na huruma
Mfano hajatokea

Mama
Mama
Kipenzi cha moyo wangu

Faraja ya moyo wangu
Kipenzi cha roho yangu
Amenikirimu mungu
Ni mama
Ni mama
Ni mama
Ni mama

Ufunguo wa maisha yangu
Na dhamana ya pepo yangu
Ni mama

Faraja ya moyo wangu
Kipenzi cha roho yangu
Amenikirimu mungu
Ni mama

Hata ukiwa na dhiki
Mama yako hakutupi
Kukucheka hadiriki
Ni mama

Hata ukiwa na dhiki
Mama yako hakutupi
Kukucheka hadiriki
Ni mama

Haijalishi ntavokuwa
mama utanipokea
Mzuri au mbaya
Wewe hutonibagua

Haijalishi ntavokuwa
mama utanipokea
Mzuri au mbaya
Wewe hutonibagua

Chuo changu cha kwanza
Ni wewe wangu mama
Maadili umenifunza
Ili niwe mtu mwema
Maadili umenifunza
Ili niwe mtu mwema

Rabbi umrehemu daima mama yangu
Kila lake gumu
Mfariji mola wangu
Mama yangu umrehemu
Nakuomba Mola wangu



Credits
Writer(s): Mubarak Atigh
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link