Wimbo Usio Bora

Rudi nyumbani kapumzike
Rudi nyumbani kapumzike
Nimeshindwa na maudhi
Rudi nyumbani kapumzike
Ukishabadilika utarudi
Maana haya mahusiano yananipoteza
Haya mahusiano yananipoteza
Najua we' ni mrembo na machoni unapendeza
Ila una haraka na kwenda na kasi yako sitaweza

Umeanza kuigeza jinai
Eti nipate nguvu unanilisha pweza na chai
Haujui habari ulizosoma zimewekwa masilahi
Umeshika simu sana mpaka umenipoteza walahi
Ukiona mashati mabuti unapagawa
Na miili ya movie ambayo wame-boost na madawa
Unataka niache kazi na mimi nishinde gym niji-boost
Eti niwe kama Jux unanigawa
Umepumbazwa hutaki shika kisomo
Unakubali kila kitu hujui mengine ni promo
Nilikuwa nakuridhisha leo unataka nikuridhishe
Mara mbili kwa kunifananisha na wacheza ngono
Unaniambia sinukii fresh inanilazimu
Ninunue marashi ya gharama toka Zenji
Toka enzi, nahisi mpenzi una wazimu
Unanidharau sababu ya maisha unayo-check kwenye simu
Haki ya mama ukweli, uwongo sibongi
Tangu umepata hiyo simu msosi boko sikosi
Usiku mzima una-chat kelele ndoto sioti
Eti unajiita princess Jojo kidoti
Kwanini usiache drama tuishi ka' zamani?
Hizi kashikashi zinanichanganya
Mara unilambe mara utake ku-kiss hadharani
Kisa kina flani walifanya
Ushanitia nuksi tangu tanga zama
Tungeweka kifusi cha mchanga ukachagua harusi ya kisasa
Ukalia machozi nikavunga nikakusikiliza
Mpaka sasa tunaishi kwenye nyumba ya kupanga
Kisa unasema dunia tunapita mpango gani huu
Ndani hatuna hata akiba ya pesa ni vidani tu
Sitasahau siku madeni ya harusi bado sijalipa
Ukalazimisha nikope ili twende honeymoon
Honeymoon
Huu upendo unaniliza ah!
Huu mwendo umenishinda
Nimepaka rangi upepo nimekupenda wewe
Wakati unapenda urembo kupitiliza
Nimegundua hii hujuma sitanyamaza
Mpaka sipeleki tena huduma tena kwa maza
Baada ya miaka kadhaa ya kwenye nimegundua
Huu upendo wangu unanilemaza
Zikwapi enzi zako
Kazi umefukuzwa maana masihara yameshusha weredi wako
Njaa ikija tuuze hereni na cheki zako
Au tuuze samani ili kulipa madeni yako
Kutumia pesa za akiba ndio wazimu kabisa
Kodi ikija haitalipwa na hizo timu za Twitter
Mke wangu umejua jiji, mpaka najiuliza
We ni nani? Kwa maana mke wangu hakua hivi
Nimeshachoka ona sura yangu inajieleza
Wakati nakuoa tabia yako ilipendeza
Namtaka mke wangu wa mwanzo yule niliyempenda
Sio huyu anayemsalimia maza kwa kiingereza
Vile unaniona mpole unajivika mapembe
Nilikupa uhuru sasa unanishika makende
Hii tabia uliyoianzisha inanisikitisha na nimeshindwa
Sa' nazila nisepe
Angalia rafiki zangu, kisha linganisha na rafiki zako
Hasa ambao wanaomzunguka binti yangu
Huwa nawaza wanachomfundisha ni nini?
Zaidi ya umbea kunywa pombe na kupiga vimini
Mama hao rafiki zako washaoza
Hakuna afadhali hata mmoja
Wanapenda sana maisha ghali nilikupa taadhali ukae mbali
Hukukubali, yule mrefu alishawahi kunitongoza
Anajua nimekuoa nimefunga mageti yangu
Nisingemkubali hata angenikuta enzi zangu
Ananishika kila akinikuta peke yangu
Anasema umemwambia kuhusu ukubwa wa nyeti zangu
Asa' ndo' nini? Sijui Kuruthumu sijui Martha
Mrefu mweusi yule mwenye tatoo kwenye paja
Ni mpumbavu sana anajikuta anajua
Ana mdomo mchafu sijui ka' anaulia chakula
Mbele ya mtoto anatukana ka' pepo
Anajua viungo vyote maana alishalala hadi central
Kila mtoto wetu huwa napata mateso
Unataka tulee mtoto au malaya wa kesho
Wema hauna gharama mahususi
Ila pindi unapotenda ubaya
Jua ubaya utarudi hauwezi kuitabili kesho hata uwe special
Dunia duara mama acha kujifanya mjuzi
Siku ambayo yatakuhama makundi
Na mimi nitaumwa sana niko ndani nimelazwa mahututi
Na pesa hamna ya kununua kiganja cha chumvi
Jirani hawezi kuja maana ushamtukana matusi
Walishasema wanazuoni "ashakum si matusi"
Si matusi mke wangu, walishasema
Nyuma ya mwanaume masikini kuna
Mwanamke mpumbavu
Pesa tulizopoteza sio kinachoniuma
Pesa zipo na zinatafutwa
Sio gari, sio nyumba kinachoniuma
Umenipotezea time na siwezi kuurudisha muda
Umeiweka kweli sababu ya maisha ya ndoto
Umekumbatia uongo unaishi kama mtoto na
Umekua umefungua milango ya kejeli
Elimu ya jando na unyago zimefeli

Rudi nyumbani kapumzike
Rudi nyumbani kapumzike
Rudi nyumbani kapumzike
Ukishabadilika utarudi



Credits
Writer(s): Edger Vicent Mwaipeta
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link