Kesho

Kesho nafasi ya kuanza upya
Kumaliza kuishi nafasi ya kuanza kufa
Kuivunja sheria nafasi ya kufuata ruksa
Kuikumbuka jana au kuanza kuifuata future

Future ni leo siku ambayo miti hukimbia
Jua hushuka upendo, marafiki hufifia, [hufifia
Wimbi la wanafiki huingia
Kesho ya tumaini hubakia

Tumaini, shika walau shika walau
Na ujifunze kuziba kombe pindi anapopita nyang'au
Akishapita tenda wema halafu kisha sahau
Na uchunge unaponena watakuzika wadau

Wadau, walikua uchi ukawavika mavazi
Nyumba yako ikavunjika wakakunyima hifadhi
Je, utasamehe utasahau kulipa kisasi
Au kesho itakukuta umeshika risasi

Risasi inawaza wapi itakukutia kesho
Utatoroka kambi ama utavungia ghetto
Tusipofikia lengo, utahama ukoo kwa kitu kidogo au utaitumikia nembo

Nembo ya mjeshi ninayekaza mwendo kishujaa
Kama unavyokaza nyonga kwenye tendo la zinaa
Napiga goti nashukuru uwepo wa sanaa
Kihisia nawapeleka kesho majamaa
Majamaa walikua wavivu hawakukazana
Waliishia kuamini kuwa kuna wingu la laana
Waliseti mipango ila siku hazikufanana
Huwezi kuikabili kesho kwa mbinu za jana



Credits
Writer(s): Edger Vicent Mwaipeta
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link