Fumbo Mfumbie Mjinga

Fumbo mfumbie mjinga
Mwerevu! Mwerevu hutambua
Fumbo mfumbie mjinga
Mwerevu! Mwerevu hutambua

Wanifumbia mafumbo
Ukiniona huna raha
Wanifumbia mafumbo
Ukiniona huna raha

Watamani kuniua, kuniua!
Watamani kuniua, kuniua!

Je, nimekuibia mumeo? Sema! Sema!
Je, nimekuazima nguo? Sema! Sema!
Je, nimekuomba chakula? Sema! Sema!
Je, nimekuazima mapambo? Sema! Sema!

Bibie, unikome!
Unikome! Nakuambia, unikome!
Bibie, unikome!
Unikome! Nakuambia, unikome!

Wachemshe hao hao, wachemshe hao hao
Wachemshe hao hao Kwangu mimi utapoa!
Majungu hapo ndiyo kwao
Majungu hapo ndiyo kwao
Majungu hapo ndiyo kwao
Hasidi usiyojijua

Wachemshe hao hao, wachemshe hao hao
Wachemshe hao hao Kwangu mimi utapoa!
Majungu hapo ndiyo kwao
Majungu hapo ndiyo kwao
Majungu hapo ndiyo kwao
Hasidi usiyojijua

Mimi si mke mwenzio, chuki usiniwekee
Usiniwekee vikao, yangu kuyafuatilia
Mimi si mke mwenzio, chuki usiniwekee
Usiniwekee vikao, yangu kuyafuatilia
Mimi si mke mwenzio, chuki usiniwekee
Usiniwekee vikao, yangu kuyafuatilia
Mimi si mke mwenzio, chuki usiniwekee
Usiniwekee vikao, yangu kuyafuatilia

Bibi, wacha ushambenga
Losh! Mzushi wewe
Professor wa kuzua
Losh! Mzushi wewe
Professor wa kuzua
Si hayo tu, na mengine mtazusha
Ya fitina na majungu, kwangu utagonga mwamba
Si hayo tu, na mengine mtazusha
Ya fitina na majungu, kwangu utagonga mwamba
Usinitafute undani, ya kwako yamekushinda
Ya kwako yamekushinda, yangu utayaweza?
Usinitafute undani, ya kwako yamekushinda
Ya kwako yamekushinda, yangu utayaweza?
Ya kwako yamekushinda, yangu utayaweza?

Usinizeeshe mwenzio, usinizeeshe mwenzio
Usinizeeshe mwenzio, midomoni kunitia
Sitembei na mumeo, sitembei na mumeo
Sitembei na mumeo, ndereje kunichukia
Usinizeeshe mwenzio, usinizeeshe mwenzio
Usinizeeshe mwenzio, midomoni kunitia
Sitembei na mumeo, sitembei na mumeo
Sitembei na mumeo, ndereje kunichukia

Mchimbo bibi hashuo, uongo kunizulia
Kuninanga mwisho leo, uongo kunizulia
Mchimbo bibi hashuo, uongo kunizulia
Kuninanga mwisho leo, uongo kunizulia
Mchimbo bibi hashuo, uongo kunizulia
Kuninanga mwisho leo, uongo kunizulia
Mchimbo bibi hashuo, uongo kunizulia
Kuninanga mwisho leo, uongo kunizulia
Nitue mwana mwenzio
Losh! Mzushi wewe
Professor wa kuzua
Losh! Mzushi wewe
Professor wa kuzua

Si hayo na mengi utayasema
Ya umbea na fisadi, kwangu utagonga mwamba
Si hayo na mengi utayasema
Ya umbea na fisadi, kwangu utagonga mwamba
Uso haya ujionii, mafumbo yako ya nini?
Uso haya ujionii, mafumbo yako ya nini?
Ahh Mafumbo yako nini shangingi ushaishiwaa
Mafumbo yako nini shangingi ushaishiwaa

Sitaki! Sitaki maneno na wewe!
Sitaki! Sitaki kukaliwa mwao
Sitaki! Sitaki maneno na wewe!
Sitaki! Sitaki kukaliwa mwao
Wewe unawako, na mie nina wangu
Maneno ya nini?
Wewe unawako, na mie nina wangu
Maneno ya nini?
Sitaki mafumbo kunifumbia mwenzio
Sitaki mafumbo kunifumbia mwenzio

Wewe una nyimbo, mwenzio nina mambo
Rusha roho za nini?
Wewe una nyimbo, mwenzio nina mambo
Rusha roho za nini?

Ukome ukware, kuharibu hadhi yangu!
Ukome ukware, kuharibu hadhi yangu!
Bure kiherehere, hutakiwi kifagio
Kimuhe-muhe cha nini?
Bure kiherehere, hutakiwi kifagio
Kimuhe-muhe cha nini?



Credits
Writer(s): Chamazi Music
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link