Acha Wee Taarab

Utapanda na kushuka na watu kunitumia
Utapanda na kushuka na watu kunitumia
Bure utafedheheka na aibu kujitia
Bure utafedheheka na aibu kujitia
Najuwa najuwa unanitaka moyoni
Moyoni unaumia
Najuwa najuwa unanitaka moyoni
moyoni unaumia
Ukweli wangu hakika
Ukweli wangu hakika
Ukweli wangu hakika
wewe hujanivutia

Acha wee Acha wee Acha wee
Suti gani nazo za kuazimisha
Acha wee Acha wee Acha wee
Nayako mabobish yananichekesha
Acha wee Acha wee Acha wee
Huishi mitaani unajitakisha
Acha wee Acha wee Acha wee
Akutake nani kumkorofisha

Unakoroga najua, nawatu wameshakushuku
Unakoroga najua, nawatu wameshakushuku
Bure unajisumbua, kujivunjia sharafu
Bure unajisumbua, kujivunjia sharafu
Yuko yuko anaeniuwa
Mwenye mwenye njema insafu
Aaah Yuko yuko anaeniuwa
Mwenye mwenye njema insafu
Roho anaenitoa
Roho anaenitoa
Roho anaenitoa
Roho anaenitoa
Kwake yeye hufui dafu

Acha wee Acha wee Acha wee
Suti gani nazo za kuazimisha
Acha wee Acha wee Acha wee
Nayako mabobish yananichekesha
Acha wee Acha wee Acha wee
Huishi mitaani unajitakisha
Acha wee Acha wee Acha wee
Akutake nani kumkorofisha

Bure unajivalisha masuti yenye thamani
Bure unajivalisha masuti yenye thamani
Nyengine waazimisha kurandia mitaani
Nyengine waazimisha kurandia mitaani
Hima Hima unajitakisha
Asubuhi asubuhi na jioni
Hima Hima unajitakisha
Asubuhi asubuhi na jioni
Ni kachara umekwisha
Ni kachara umekwisha
Ni kachara umekwisha
Ni kachara umekwisha
hunifai asilani

Acha wee Acha wee Acha wee
Suti gani nazo za kuazimisha
Acha wee Acha wee Acha wee
Nayako mabobish yananichekesha
Acha wee Acha wee Acha wee
Huishi mitaani unajitakisha
Acha wee Acha wee Acha wee
Akutake nani kumkorofisha

Mimi ninaemtaka sharti awe dogodogo
Mimi ninaemtaka sharti awe dogodogo
Anotizamika na fedha japo kidogoo
Anotizamika na fedha japo kidogoo
Huniwezi huniwezi si dhihaka
Huiwezi huiwezi mititigo
Huniwezi huniwezi si dhihaka
Huiwezi huiwezi mititigo
Usinivishe cha ukoka
Usinivishe cha ukoka
Usinivishe cha ukoka
Usinivishe cha ukoka
Kilemba bwana mdogo

Acha wee Acha wee Acha wee
Suti gani nazo za kuazimisha
Acha wee Acha wee Acha wee
Nayako mabobish yananichekesha
Acha wee Acha wee Acha wee
Huishi mitaani unajitakisha
Acha wee Acha wee Acha wee
Akutake nani kumkorofisha



Credits
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link