Mkuu

Ukuu ni wako, ee Mwenyezi-Mungu,
Una nguvu, utukufu, ushindi na enzi.
Vyote vilivyoko mbinguni na duniani ni vyako.
Mwenyezi Mungu, ufalme ni wako, nawe umetukuzwa,

U mkuu juu ya vitu vyote
Utajiri na heshima hutoka kwako, vyote wewe wavitawala
U mkuu juu ya vitu vyote

Uwezo na nguvu vimo mkononi mwako
Nawe Bwana, wawakuza uwapendao,
Na huwaimarisha wote, ee Bwana
Sasa ee Mungu wetu, twakushukuru na kulisifu Jina lako
Jina lako tukufu

U mkuu juu ya vitu vyote
Utajiri na heshima hutoka kwako, vyote wewe wavitawala
U mkuu juu ya vitu vyote

(Watawala)
U mkuu juu ya vitu vyote

(Jina Lako Yesu lapita majina yote)
U mkuu juu ya vitu vyote



Credits
Writer(s): Cor Akim
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link