Nini Nitafanya

Weekend niko zangu ghetto nakula ngoma za town
Pembe glass ya juice nashushia na popcorn
Tryna get away uchov na mishe za mjini
Nikapitiwa na usingizi baada ya ngoma kuingia Kichwani
Naamshwa kwa mlio wa simu saa 12 jioni
"Yo papi zipi za wapi unafanya nini?"
"Nimepoa ghetto Inno nimechoka ile mbaya man"
"Acha uzembe jisogeze location B Baharini"
"Give me forty five minutes am gonna be there mine"
Nkanyuka baada ya kubath, vuta ndinga barabarani
Nikatimba location B baada ya dakika thelathini
Nikamvutia waya mchizi "yo man maeneo gani"
Akanielekeza mchizi nikatimba aliketi na bonge la Queen
Akanitambulisha kwa shemeji kwa jina anaitwa Suzan
Tukaendelea kula bata nikawaacha mi nikasepa
Usiku wa pili baada ya weekend nipo ghetto nakamua
Simu ikaanza ita namba ngeni nikaichunia
Ikaita nikaichunia ikaita tena nikaipokea
"Hello, Mambo dear"
"Poa, Nani ananongea"
"Otea"
"Sina idea"
"oooh, Suzy dear. Hii ni namba yangu usiache kunipigia"
Akakata nami nkavunga akanitext night night dear

Baada ya wiki moja kupita mchizi Inno akanipigia
"Yoo Bro vp upo ghetto mi na Suzy tunakutimbia"
Wakatia maguu ghettoni, midamida wakapepea
Jmosi inayofata motto Suzy akanitembelea
Meen, alikuwa amewaka kinyama unaweza sema Malkia
Kwa kochi pozi uchokozi suddenly akanisogelea
Unga ukazidi maji ndimi kwa ndimi mambo yeah
Akapandisha yake mini na brauzi yake akaivua
Kwa nje motto balaa akiwa naked ndo balaaaa
Nikavuta tata nikachapa kiplay boy giza likaingia
Kwa ufundi akagoma sepa all the night ile hahaaa
Suzy akaendelea, nikaanza juta udhaifu wangu na tamaa
Inno mwanangu sana nitawezaje kumuangalia
Nikamcheki Inno kwa line, nikamtonya Suzy mafua
"Mafua wapi babu acha zengwe au kaka umekolea?"
Nikashindwa kumsimulia cause kinyama anamzimia
Suzy akazidisha fujo eti hajutii kilichotokea
Akataka kumuacha mchizi sababu yangu kwake poa
Nkamtonya asahau kuhusu mimi sababu Inno anamzimia
Akasema nikizidi kumkataa Inno atamwambia
Akasema "Nataka uje kuniona ila kwanza mimba ntakubebea"
Mpaka leo najiuliza nini mchizi nitafanya
Nimwambie mwanangu ukweli kisha nikubali lawama
Au nikaushe tu, je siku akijua nini nitasema
Kwa jinsi mwana alivyokolea kwa huyu binti asee mpaka huruma
NINI NITAFANYA?

Haikuwa nia yanguuuu Yeeeeee eeee eeee
Kumsnitch mwanangu mwanangu oooo whyyyyyyyy
Sijui ni shetaniiii, hizo mambo gaaaniii
Ila Mwanangu samahaniii eoooooooo



Credits
Writer(s): Rashid Ally
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link