Badman

Aah aaaah
Phonse on the beat fire

Me sio mwanaume wa paga wala so mwanaume wa shoka
Ila nina roho mbaya mpaka wachawi wananiogopa
Kwangu mke bora anapatikana kimboka
Nishawahi fanya balaa mpaka shetani anaogopa

Nishauwa sana panya bila kutumia sumu
Nishatumiaga beseni kubeba majukumu
Mwenzenu kumpiga bosi kwangu sio kazi ngumu
Mtoto wa miaka miwili namvutisha ndumu

Yaani naogopwa kama kelele za mwizi
Ukipanga kuniroga jua uniroge chizi
Kwenye bwawa la mamba mi napiga mbizi
Na nikifa siachi pengo naacha fizi

Oya mi mtu mbad
Wanangu mi mtu mbaya
Oya mi mtu mbad
Wanangu mi mtu mbaya

Hata ukienda kwa mganga kutambika jina langu
Atakujibu nishazikwa we soma matanga
Kisha niibuke na wanangu
Tunakula kitakachopikwa

Njia nilizopita hazinaga mfano
Mwenzako nimeshapita hadi tundu la sindano
Lengo kutimiza ndoto na sio mashindano
Ndomana nawasha moto na sina mfano

Sina tatizo na waliopanga kunikomoa
Nawasalimu walosema sitatoboa
Mtaani ngoma zina hit mpaka zinaboa
Tena siimbi sana na smoke na kukohoa

Mimi ni kioo nitazane ujione
Ukiweze ninachofanya hebu fanya tuone
Aidha ufe upone sina dhihaka hata tone
Na ukijifanya unanijua mi sitaki unione

Oya mi mtu mbad
Wanangu mi mtu mbaya
Nasema mi mtu mbad
Oya mi mtu mbad

Phonse on the beat fire
Afrizon



Credits
Writer(s): Erick Gift
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link