Kadadaa

Uuuh turururuuruu rururuu ruruuuuu!

Nakosa raha, kila ninachofanya unakataa!
Kutwa karaha, wangu Mollah niepushe na mabalaa!
Aah hivi mi nilikosa nini Habibty sema!
Utulie kwangu nikuvishe Pete chanda chema!
Napenda kupendwa sana, we usijenikana!
Mi nishatendwa sana, usiniache bwana!
Aah kweli vijana wengi wa sasa wanadanganya!
Lengo wakuvuruge tu ka-danadana!

We ndio unanifaa we unanifaa changu kifaa!
Basi we nipe raha we nipe raha mie mateka!
Rahaa!

Sijui ni nini madrashki vitimbwi yaani kila kitu!
Baki na mimi nikupe penzi ujinga sithubutu!
Mpenzi unanionea kutwa kukicha sili silali mawazo!
Mi nalia milima mabonde mi kwangu vikwazo!
Ah mapenzi mapenzi yanaumiza moyoni!
Mwenzako siwezi mbele Kiza sioni!
Aah kweli vijana wengi wa sasa wanadanganya!
Lengo wakuvuruge tu ka-danadana!

We ndio unanifaa we unanifaa changu kifaa!
Basi we nipe raha we nipe raha mie mateka!
Rahaa

Shuruba shuruba nibalaa!
kwanini wafanya mwenzako nachakaa!
We nipoze ka-moyo Kadadaa!
Kuwa na moyo wa huruma usije kukataa!
Shuruba shuruba ni balaa!
We nipoze kamoyo Kadadaa!

Ha ha ha!
Ya dun know!



Credits
Writer(s): Shabani Shabani
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link