Yatapita

Yatapita yana mwisho
Ipo siku tutayasahau
Watatuheshimu walio tudharau
Kaza moyo, nivumilie
Amini tutayasahau
Watatuheshimu walio tudharau (Wote)
Na ntakununulia (Vyote)
Mawigi na simu (Vyote)
Ntakuzawadia (Vyote)
Pochi zenye thamani (Vyote)
Nawe uende waringishia (Vyote)
Utembee kwa uskani (Vyote)
Na vioo ukiwafungia (Vyote)

Aloiumba leo ni mungu na ndio ataiumba kesho
Amini fungu letu laja haliko mbali
Alisema mtazaa kwa uchungu, tutatafuta kwa mateso
Baby mitihani kawaida usijali, mnh!
Kidogo nnachokuletea usinune pokea
Nipate moyo nifariji
Na juhudi naziongezea usichoke niombea
Molah atubariki zaidi
Mungu kakupa sura kakupa shepu
Nyuma chura mambo yetu
Mwana wa sanura, mwenzako mimi, I love you
Umeniteka medula niko fyetu
Akili haina ndala iko peku
Umenivurura, mwenzako mimi, I love you
Ooh nivumilie

Yatapita yana mwisho
Ipo siku tutayasahau
Watatuheshimu walio tudharau
Kaza moyo, nivumilie
Amini tutayasahau
Watatuheshimu walio tudharau (Wote)
Na ntakununulia (Vyote)
Mikufu na simu (Vyote)
Ntakuzawadia (Vyote)
Pochi zenye thamani (Vyote)
Nawe uende waringishia (Vyote)
Utembee kwa uskani (Vyote)
Na vioo ukiwafungia (Vyote)

Ooh Baby
Tazama Nyota na Mbalamwezi zatutazama
Liliwaka jua zikafanya subira mnh! nhh!
Na nnapokosa niambie mupenzi sio kuzozana
Nyumba haijengwi kwa vita hasira
Kwenye macho yako nikiyatazama
Naiona huruma yako mama
Changamoto maana kuna muda unakata tamaa
Nanoa kisu hatuli nyama
Na kodi lundo zatuandama
Riziki zama kwa zama
Ya kwetu kesho ya kwao ni jana
Kidogo nnachokuletea usinune pokea
Nipate moyo nifariji mnh!
Na juhudi naziongezea usichoke niombea
Molah atubariki zaidi
Yatapita kipenzi changu

Yatapita yana mwisho
Ipo siku tutayasahau
Watatuheshimu walio tudharau
Kaza moyo, nivumilie
Amini tutayasahau
Watatuheshimu walio tudharau (Wote)
Na ntakununulia (Vyote)
Mawigi na simu (Vyote)
Ntakuzawadia (Vyote)
Pochi zenye thamani (Vyote)
Na wewe uende waringishia (Vyote)
Utembee kwa uskani (Vyote)
Na vioo ukiwafungia (Vyote)

Mungu kakupa sura kakupa shepu
Nyuma chura mambo yetu
Mwana wa sanura
Mwenzako mimi, I love you



Credits
Writer(s): Nasibu Abdul Juma Issaack, Siraju Hamisi Amani
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link