Ua Langu

Pale niki' kutazama
Yanawiri macho yangu
Moyoni hua nahema
Ukiniita jina langu
Hubani kwako nazama
Niokoe habibti wangu

Asubuhi ni jua lako
Nikumulike usoni
Niangaze mwezi wako
Usipotee gizani
Unifanye nyota zako
Zing'arazo angani

Kidole chako cha pete
Nitakuvisha johari
Uwendapo tuwe wote
Tuwe sote ng'ari ng'ari
Wabaya wasikufate
Nitakulinda vizuri

Ua langu la waridi
Zuri lenye kusifika
Naapa nakuahidi
Siwezi kukuepuka
Mola wangu ni shahidi
Nifapo utanizika

Uwepo wangu ni wako
Uwendapo nitakuja
Furaha yangu ni yako
Roho ziwe na faraja
Niweke moyoni mwako
Daima tuwe pamoja

Ni lazima nikupende
Hilo wazi nalijua
Nawe pia unipende
Hilo ni lako tambua
Mimi nikulishe tende
Nawe nilishe halua

Kutoka nilipo kuona
Moyo umekupenda
Nimekosa La kufanya
Umekuwa wangu nyonda
Daima nitakutunza
Ewe habibati

Ua langu la waridi
Zuri lenye kusifika
Naapa nakuahidi
Siwezi kukuepuka
Mola wangu ni shahidi
Nifapo utanizika



Credits
Writer(s): Abubakar Salim
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link