Asante

Uliniumba kwa sura Yako
Ukanipa upendo Wako
Sikukosa kitu Kwako
Ila Nikakuangusha Bado
Uliweza umba mwingine
Akutii na akuheshimu
Ila ulinipenda bado
Na ukanipa nafasi nyingine

Asante Baba
Asante Yesu
Asante Baba
Asante Yesu
Uuuuh Asante

Ninapokuwa na kiu
We ni maji ya uzima
Ninapokuwa na njaa
We mkate uzima
Ninapoona mashaka
Wewe kwangu msaada
Na mawimbi yakivuma
We mtuliza dhoruba
Nitatoa nini kwako Baba
Kilicho zaidi ya pendo Lako

Asante Baba
Asante Yesu
Asante Baba
Asante Asante Yesu
Uuuuh Asante

Baba Asante
Kwa wema Fadhili
Asante
Umetenda mengi kwangu
Asante
Na Kwa yote unipayo
Asante
Hata gumu lije kwangu
Asante
Ninajua utatenda
Asante
Asante Yesu Asante Yesu
Ninashukuru
Asante



Credits
Writer(s): Happiness Josiah
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link