Safari ya Ushindi

Basi Imani chanzo chake
Ni kusikia na kusikia
Huja kwa neno la Kristo
Tuliposikia neno lako
Tulikuamini
nawe ukatupokea
Ukatusamehe dhambi
Na kutufanya wana wako
Na hii ndio ujasiri wetu kwamba
Lolote tuombalo kwa jina lako
We utafanya maana kila aombaye
Hupewa na atafutaye ataona na
Kila abishaye kwako atafunguliwa
Ni maombi yetu siku ya leo
Utuongezee Imani Bwana
Hata wale wasiokuamini wewe
Walisikie neno lako
Wakuamini, watubu na
Waokolewe eeh maana
We Bwana hukawii kutimiza
Ahadi yako kama wengine
Wanavyodhani na hupendi
Yeyote yule apotee
Bali wote waifikirie ile toba
Na huu ndio ushindi wetu

Hii ndio mbegu iliyopandwa
Katikati ya jangwa

Huu ndio mlima waliosema
Hatuwezi kuupanda

Hii ndio bahari waliosema
Hatuwezi ivuka

Hii ndio imani inayoweza
kuhamisha milima

Hii ndio mbegu iliyopandwa
Katikati ya jangwa

Huu ndio mlima waliosema
Hatuwezi kuupanda

Hii ndio bahari waliosema
Hatuwezi ivuka

Hii ndio imani inayoweza
Kuhamisha milima

Na habari njema siku ya leo
Ni kwamba Yesu mwenyewe
Ndiye mwokozi wetu na
Katika mambo yote
Tunashinda na zaidi ya
Kushinda kwake yeye
Aliyetupenda na tena
Hakuna chochote cha
Kututenga na upendo wake
Yesu eeh

Maana kama ni mateso
Tuliteseka pamoja naye na
Tuhai leo, sio sisi tulio hai
Bali Kristo yu hai ndani yetu
Ikiwa ni majaribu hakuruhusu
Tujaribiwe zaidi ya Imani
Zetu oh, na pale alipoona
Majaribu yanazidi kuwa
Makubwa bado mwenyewe
Alifanya mlango tukatoka
Salama kwa ushindi ile
Hesabu ya majeraha na
Maumivu yetu ndio iliyofanya
Kikombe chetu cha ushindi
Kikafurika eeh

Ni kama tu mateso ya Kristo
Pale msalabani kadri
Alivyokuwa akisulubiwa
Haikumfanya aonekane
Kama ameshindwa bali
Ilichochea kuleta ukombozi
Kwa ulimwengu mzima
Mimi na wewe leo tumepona
The harder the battle
The sweeter the victory
We are victorious through
His name and this is
Victorious journey

Hesabu ya jeraha zetu
Ni hesabu za ushindi wetu
Safari ya ushindi
Safari ya washindi

Tuliyenaye Safarini
Uhakika tunao
Kiongozi wetu ndiye
YESU mwenyewe

Hesabu ya jeraha zetu
Ni hesabu za ushindi wetu
Safari ya ushindi
Safari ya washindi

Tuliyenaye Safarini
Uhakika tunao
Kiongozi wetu ndiye
YESU mwenyewe

Katubeba
Hatuanguki kamwe
Katubeba
Hatuanguki kamwe
Katubeba
Hatuanguki kamwe
Katubeba
Hatuanguki kamwe

Ooooh...



Credits
Writer(s): Neema Choir
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link