Fundi Ni Yatima

Ninao msiba
Fundi ni yatima
Kila nikondapo huwaza mengi
Kisa ni cha baba na mama
Baba na mama wako ahera

Haikuanza sasa
Ni kupungukiwa
Ndugu zangu wengi kunipotea
Waume kwa wake hunigura
Si amri yangu ni ya mola

Walizaliwa kumi
Wa moja ni mimi
Sita walikwenda hali ni wadogo
Waume watatu na dada zao
Tulibaki watatu na wanawake ni wawili

Juzi haikutosha
Mmoja alikwenda
Sasa tulobaki hesabu sawa
Wakwanza nami wamwisho tu waume
Wapili kwa kuzaliwa na mdogowe ni wanawake



Credits
Writer(s): Fundi Konde
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link