Tenda Wema

Woi woi woiee... nenda
Tenda wema nenda zako... nenda
Usingoje kusifiwa mama wee
Usisubiri asante ...nenda
Usingoje shukrani mama wee.nenda
Wanadamu si wema mama wee
Wana meno wanauma mama wee
Wanawasha kama pilipili mama wee
Wanaupupu utajikuna wee mama
Meno yao kama chumaaa... mama wee
Tenda wema nenda zako utalipwa na Mungu
Ukisubiri kusifiwa mama we
Ukingoja shukurani mama wee.mama
Makubwa yatakukuta mwenzangu wee
Makubwa yatakukuta pole we
Matusi utayasikia pole wee
Dhihaka utazitambua mama wee
Kachiba utatupiwa mama wee
Tenda wema nenda zako mama
Nasema usigeuke nyuma ...nenda mama
Nenda... nasema nenda... aaah nenda utalipwa na Mungu
Siku ya mateso yako pole wee
Siku ya mateso yako mama wee pole wee
Siku ya huzuni yako mama
Siku ya mahangaiko yako mama we
Siku ya anguko lako mama wee... pole wee
Waliokuwa rafiki zako mama
Watageuka mwiba kwako polee
Waliokula chakula chako mama
Watageuka anguko laako mama wee polee
Uliotenda wema kwao pole wee
Yatageuka maumivu yako polee
Waliokula chakula chako... siku ile
Watasahau wema wako mwenzangu wee
Watakaa vibarazani jamani eee
Watacheka na vicheko mama wee
Majina watakupatia pole wee
Tena mabaya yenye hatia tena
Mabaya yenye udhia kwako
Watakuita kimbelembele kimbelembele
Ati wewe kimbelembele mwenzangu kimbelembele
Wema wako kimbelembele kimbelembele
Uliwasaidia kimbelembele kimbelembele
Uliwasaidia kimbelembele ati wewe kimbelembele
mama mama... mama wee mama mama
Usichoke kutenda mema utalipwa na Mungu
Wacha niseme ukweli jamani ee
Wacha niseme ukweli mwenzangu wee
Wanadamu hawabebeki hawabebeki
Hata ukifanya nyinyi hawabebeki
Wabebe kwa mbeleko ya chuma... hawabebeki
Wabebe kwa maturubai .hawabebeki
Watachukua na viwembe jama ee mama
Watachana turubai kweli
Wachane wakukimbie pole wee
Wabebe kwa mbeleko ya chuma hawabebeki
Watatafuta misumari jama ee mama
Watagonga ngo ngongo ngongo ngongo
Wape chakula wale haya washibe wakutukane jama ee mama
Wape chakula wale tena kesho watakushitaki mama wee
Nenda nenda... aah nenda utalipwa na Mungu(uuuuuu)
Mukama kwange kwagara kwagara
Mwami wanje kwagara kwagara
Mukama kwange kwagara nyo kwagara
Omukwano kwagara kwagara
mama mama wee... mama mama wee mama
Tenda wema nenda zako utalipwa na Mungu(uuuu)



Credits
Writer(s): Maureen Nkirote
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link