Wrong Number

Una haki sikulaumu na una kila sababu
Kuni-command, kuniuliza huyu ni nani

Siku-command mume wangu
Ila nalinda pendo langu
Upo ndani ya himaya yangu
Ndo maana nina hofu na zao langu

Mmh uko sahihi, ila inabidi uchunguze kwanza
Ukipata jibu ndo u-panic
Sio tu kuwa unavimba

Hayo si maneno mume wangu
Kuyanena mbele yangu
Unazipelekea hisia zangu
Kuhisi naibiwa zao langu

Mmh basi baby, nakupa message usome
Na ukishasoma, usilalamike

Usini-set mume wangu
Nataka kuipoza roho yangu
Suluhisho la moyo wangu
Mpigie upoze mtima wangu

Tusigombane kisa message hiyo
Baby sijui, amekosea namba
Haipaswi kulalamika

Haiwezekani tumpigie
Tuweke loud speaker tumsikie
Haiwezekani akosee namba
Wakati wenye simu ni wengi

Tusigombane kisa message hiyo
Baby sijui, amekosea namba
Haipaswi kulalamika

Haiwezekani tumpigie
Tuweke loud speaker tumsikie
Haiwezekani akosee namba
Wakati wenye simu ni wengi

Chozi langu thamani, lanitoka chumbani
Namlilia nani? Kama si wewe!

Ninajua ni hasira, zikipoa mpendwa utaelewa
Hata maji ya moto, hupoa mapema yakipepewa

Usipoteze lengo mume wangu
Wataka kuzifumba mboni zangu
Mpigie huyo mwenzangu
Ili nijue kuwa siko peke yangu

Mmh haya kachukue charger yangu
Ipo kule kwenye mkoba wangu
Ukisharudi tena kwangu
Wewe utafurahi mke wangu

Tusigombane kisa message hiyo
Baby sijui, amekosea namba
Haipaswi kulalamika

Haiwezekani tumpigie
Tuweke loud speaker tumsikie
Haiwezekani akosee namba
Wakati wenye simu ni wengi

Uuh! Ona sasa, zimefutika namba
Zimefutika sms kwenye inbox!

Hapana baba, umezifuta makusudi
Mbona mi mwanzo niliziona kwa macho yangu!

Tusigombane kisa message hiyo
Baby sijui, amekosea namba
Haipaswi kulalamika

Haiwezekani tumpigie
Tuweke loud speaker tumsikie
Haiwezekani akosee namba
Wakati wenye simu ni wengi
Haiwezekani tumpigie (sina namba!)
Tuweke loud speaker tumsikie (si unajua zimefutika)
Haiwezekani akosee namba (mmh)
Wakati wenye simu ni wengi

Achana nayo! (mmh sawa bwana)



Credits
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link