Yatupasa Kushukuru

Mtu mmoja alistaajabu sana, niliposema nitamshukuru Mungu
Baada ya matatizo mengi kunipata akili yangu ikampa wasiwasi
Kwa kweli nami, ilinigharimu, kujijulisha inipasavyo
Ila baada ya muda nikaona yapo mengi ya kunifanya nimshukuru Mungu

Yako mengi, hayajakwisha yatubidhishayo tumshukuru Mungu wetu
Japo twapita majaribu mengi bado, yapo mengi ya kushukuriwa
(Jiunge), he, ee, jiunge nasi, tulisisitize jambo hili la muhimu
Yale yote tujiulizayo mioyoni majibu anayo Mungu wetu

Ambassadors of Christ tuashukuru lakini kwa wengi hatueleweki
Kutokana na mambo ya yaliotupata ivi kushukuru si jambo la busara
Lakini ndugu (eh), ukitulia, nakujiuliza ya ajali ile
Tungeweza kuangamia wote kwa pamoja asiwepo hata mmoja wa kusimulia

Yako mengi, hayajakwisha yatubidhishayo tumshukuru Mungu wetu
Japo twapita majaribu mengi bado, yapo mengi ya kushukuriwa
(Shukuru), he, ee, jiunge nasi, tulisisitize jambo hili la muhimu
Yale yote tujiulizayo mioyoni majibu anayo Mungu wetu

Majaribu kama haya yalikuweko hata kwenye siku za mababu zetu
Ila kwa yote walikuwepo mashujaa walioweza kuitetea imani yao
Tuwake Mungu (eh), wakati wote, kwa yote hatujitegemei
Tukiwa hai tukiwa mauti tuwake tujualo ni moja kushukuru

Yako mengi, hayajakwisha yatubidhishayo tumshukuru Mungu wetu
Japo twapita majaribu mengi bado, yapo mengi ya kushukuriwa
(Jiunge), he, ee, jiunge nasi, tulisisitize jambo hili la muhimu
Yale yote tujiulizayo mioyoni majibu anayo Mungu wetu

He, ee jiunge nasi, tulisisitize jambo hili la muhimu
Yale yote tujiulizayo mioyoni majibu anayo Mungu wetu

Credits
Writer(s): Ambassadors Of Christ Choir
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link