Sayari

Stanza1
Sayari... sayari... eeh dunia
mbona wanipa hofu nyingi ewe dunia
yatokeao kwako ewe dunia
Kila kukicha mambo hugeuka kuwa maongo
inawezekana umezeeka dunia
au wakaao ndani yako ndio wamezeeka
Kila ufikapo ni vilio nifanyeaje
maafayawakabili wengi dunia wazeeka

Sayari dunia uliumbwa wapendeza
lakini sasa watupeleka wapi
tunahangaika hatujui tuendako
ni mungu pekee ajuaye

Stanza 2
njaa majonjwa yasiyotibika
mambo yatisha eeh dunia waenda wapi
kila mahali ni jangwa twende wapi
rotuba nayo imeshatoweka sasa twende wapi
hali ya maisha ni ngumu sana kwa wote
kwa tajiri na maskini wote nisawa
uchumi wa dunia yote wayumbaa
ona mataifa makubwa yote nayo yajejereka

sayari dunia uliumbwa wapendeza
lakini sasa watupeleka wapi
tunahangaika hatujui tuendakako
ni mungu pekee ajuaye

Stanza 3
sayari dunia umechoka
na wakao ndani yao wote wamekuchoka
hakuna mzazi awezae kuvumilia
Kuona mwanawe anakatwa kichwa kwa ajili ya kafara
damu za watu zimekua ni tamu
nionavyo si kawaida ewe dunia
tuyaonayo yanatisha dunia
oooh nahofu moyoni mwangu

sayari dunia uliumbwa wapendeza
lakini sasa watupeleka wapi
tunahangaika hatujui tuendako
ni mungu pekee ajuaye

tunahangaika hatujui tuendako
ni mungu pekee ajuaye
(repeat)
Lyrics by Ndeche Herman



Credits
Writer(s): Ambassadors Of Christ Choir
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link