Nikufahamu

Nikufahamu zaidi, Bwana
Nikujue zaidi, Yesu
Nikufahamu zaidi, ewe
Nikuishie milele, Bwana

Nataka nitembee na wewe wakati wowote
Nitembee kwa nuru yako baba
Nishirikiane na wewe kwa kila jambo
Ongoza hatua zangu ewe baba
Ongoza hatua zangu we ewe baba
Ongoza hatua hatua hatua zangu, ongoza

Wewe ni mume wa wajane
Baba wa yatima, mfariji wa waliofiwa
Mtetezi wa wanjonge
Uwaponya waliovunjwa mioyo, mioyo we
Na kuziganga jeraha zao, oh baba
Hawa wote tegemeo lao ni wewe baba, ndiposa wanasema

Nikufahamu, nikujue
(Kama Musa nionyeshe njia zako)
(Siyo matendo pekee)
(Nikae miguuni pako)
(Nikufahamu wewe)
(Nakupenda na moyo wangu wote baba)



Credits
Writer(s): Evelyn Wanjiru
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link